Friday, September 27, 2013

PEEPLES...HII NDIO MOVIE AMBAYO WIMBO WA SAIDA KALORI CHAMBUA KAMA KARANGA UMETUMIKA.

Wengi tulioangalia movie hii ya Marekani tumejiuliza wimbo wa Saida Kalori umewafikiaje.Maana ukiangalia movie hii mwanzoni mwanzoni kabisa wimbo chambua kama karanga unasikika na anaonekana mama akiucheza kama sehemu ya mazoezi.
Saida Kalori  hakua akijua chochote kuhusu nyimbo yake kutumika katika movie hiyo.Pia aliyewahi kuwa manager na producer wa Saida hakuwa akijua chochote zaidi ya kupigiwa simu kutoka Marekani na wanawe waliyoiona movie hiyo. 


Zifuatazo ni baadhi ya picha za movie hiyo







Chanzo:Dina marios, blogspot
 

Thursday, September 26, 2013

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUPAKA MAKE'UP

Vipodozi au Makeups ni urembo unaopendwa zaidi na wanawake wengi, dhamira yao ikiwa ni kubadili muonekano wao uliozoeleka ili wapendeze.

Mara nyingi watu wanapopaka makeups tofauti hujitokeza usoni kutokana na kipodozi hicho kufanya kazi ya kung'arisha na kupendezesha uso.

Unapofika wakati wa kupaka makeups,kwanza unapaswa kuchagua ni ipi itakufaa na kukupendeza. swali la kam kipi kitafaa zaidi kati ya poda au cream,hilo linabaki kwa mhusika kwa kuwa kila mmoja anapendekezo lake,kutokana namna anavyopata matokeo mazuri.


MAMBO YAKUZINGATIA KABLA YA KUPAKA MAKEUPS.

Kwanza jaribu kutafuta make ups inayoendana na ngozi yako na rangi ya mwili wako.

Watu wenye ngozi za mafuta wanashauriwa  kupaka makeup ya poda au unga unga kwani ya cream inaweza kuziba vitundu vya hewa katika ngozi ya uso.

Kwa walio na ngozi kavu wafahamu kuwa, make up ya cream haina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu katika ngozi hivyo kama unahitaji kuwa nayo kwa muda unaozidi masaa nane unapaswa kupaka makeup ya poda iliyozoeleka na wengi.

Hakikisha unapaka makeup kwa kutumia brash zake maalum na si kitambaa au mikono.

Wednesday, September 25, 2013

WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2013 WAPAGAWA NA TAARIFA YA JKT!

  HALI ya sintofahamu imewakumba wahitimu wa kidato cha sita nchini, na kuibua malalamiko miongoni mwa wahitmu hao, kufuatia taarifa iliyochapishwa na mtandao wa Jeshi la Kujenga Taifa 'JKT', ikiwataka wahitimu hao kwa ajili ya awamu ya tatu ya mafunzo maalumu, ikiwa ni mwendelezo wa program maalum ya kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wanafunzi wote wanaohitimu kidato cha sita nchini, kabla ya kujiunga na masomo yao ya elimu ya juu.

              

Taarifa hiyo, ilitanabaisha kuwa ni wito kwa ajili ya awamu ya tatu ya mafunzo hayo, ambapo wametakiwa kuwasili katika kambi walizopangiwa mnamo tarehe 28 septemba mwaka huu, ikiwa imetanguliwa na awamu ya kwanza na ya pili, zilizofanyika mapema mwezi March na June mwaka huu.



Punde tu baada ya kuwekwa kwa agizo hilo, Wahitimu wengi walionyesha kushangazwa na taarifa hiyo, ambapo walihoji ni utaratibu gani unaotumika wa kushtukiza ilihali tayari tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imeshatoa chaguzi za wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali na wapo ambao wamesharipoti kwenye vyuo hivyo.

Huku wakionesha wazi kuchanganywa na taarifa hiyo, baadhi ya wahitimu wameelezea kukerwa kwao na uchachafishaji huu uliofanywa na vyombo hivi vikubwa nchini, na kuhoji ni upi ushirikiano baina ya Tume ya vyuo Vikuu na Jeshi la Kujenga Taifa kituendaji.

Hata hivyo, wapo pia waliodai kuwa pengine taarifa hiyo ilichapishwa bila kukusudiwa kutokana na makosa ya kiufundi (technical errors), Hivyo kuwataka wahusika kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo haraka, Jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika hivyo hali ya sintofahamu kuendelea kutamalaki!
                                         
Mtandao huu ulifanikiwa kutembelea mtandao huo (www.jkt.go.tz), na kushuhudia taarifa hiyo ambayo imedaiwa kuchanganya vichwa vya wanafunzi hao, Huku wengi wao wakijiuliza, waende wapi, Kambini au Vyuoni?????

HAFSA KAZINJA AMUENZI MZEE MUHIDINI GURUMO.

MALKIA wa Zouk Tanzania Hafsa Kazinja aachia nyimbo ijulikanayo kama  “NIMUOKOE NANI” ikiwa ni moja ya njia ya kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa 1960.

Kazinja  ambaye ameibuka upya baada ya kimya cha muda mrefu katika fani hiyo  akiwa na ingizo lake la kwanza kati  ya kumi alizoziandaa kwa kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI” ambao anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.

“Nimeamua kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili  kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa wimbo wake wa “PRESHA” aliomshirikisha Banana Zorro.

Hafsa alisema  ukimya wake umetokana na kufanya utafiti na kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki na akipata mawaidha kutoka kwa wanamuziki nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo, Omar Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na kufanya naye kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni

Kazinja alisema ataitambulisha rasmi ngoma ya “NIMUOKOE NANI” katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa kufanyika OKtoba 1, 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye tamasha hilo nami naahidi kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo wasikose kuja kujionea wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake pamoja na ya ngoma zake zingine mpya"alisema.

Kazinja alisema nyimbo hiyo “NIMUOKOE NANI” ameiandaa katika studio za OM Productions ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul Salvador na Omari Mkali.

Pia Kazinja alisema alifurahishwa baada ya kupata baraka zote za kuuimba nyimbo hiyo kutoka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.

Sunday, September 8, 2013

HUYO NDIYE MWANAMKE ALIYEWEKA RECORD YA DUNIA ya KUWA NA MIGUU MIREFU KUPITILIZA.

Ama kweli ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni" Katika hali isiyokuwa ya kwaida huyu ndiye mwanamke aliyefanikiwa kuingiza katika kitabu cha kumbukumbu ya Dunia WORLD RECORD GUINESS BOOK. La kushangaza zaidi walimkutanisha na mtu mfupi zaidi Duniani.




NAMNA YA KUANDAA KEKI YA TENDE.

Unga                                   3 kikombe

Baking powder                   3 Vijiko vya chai

Sukari                                 ½ Kikombe
Tende iliyokatwa ndogo ndogo   2 vikombe

Maji yamoto                                 2 vikombe
Siagi                         4 Vijiko vya supu (au vikombe 2 vya kahawa)

Mayai                           2
Cream                              vikombe 2 Vya Kahawa

Tangawizi ya powder         2 Vijiko vya chai

Kungu manga                          1 kijiko cha chai

Mdalasini                                  1  kijiko cha chai

Hiliki                                         ½  kijiko cha chai

Vanilla                                       4  vijiko vya chai

 Vipimo Vya Karamel

Sukari ya buni (brown sugar) 5 Vijiko vya supu

Siagi                                        6 Vijiko vya supu
Lozi zilizomenywa na kukatwa
Nyembamba                                        1 kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1)   Tia maji ya moto katika tende kuiroweka kidogo.

2)   Changanya unga na baking powder vizuri katika bakuli.

3)   Tia vitu vyote vingine na uchanganye vizuri.

4)   Mimina katika bati la duara la kupikia keki ulilolipaka siagi kidogo.
    
5)   Ipikie (bake) katika moto  wa 300° kwa muda wa kama saa.

6)   Iweke katika sahani au bakuli la keki na mwagia karamel juu yake, kisha haraka upambie lozi.

 Namna ya kutayarisha Karamel
Yayusha siagi katika sufuria ndogo au frying pan kisha tia sukari ya brown.

Inapoyayuka, mwagia katika keki.

Saturday, September 7, 2013

MFAHAMU BINTI WA KIDATO CHA NNE ALIEZAA NA DIAMOND PLATNUMZ..!! DIAMOND AKANA..!!

Ni Binti aitwaye Sasha alieleza kuhusu uhusiano wake na Diamond baada ya kuungalinishwa na Binamu wa Diamond,Romey Jones ambaye alikuwa anafahamiana na Sasha huyo kabla ya Diamond.

Diamond alianza kumpenda baada ya kukutana Mlimani City kwa mara ya kwanza akiwa na rafiki zake na uhusiano wao uliendelea mpaka alipofanikiwa kumpata mtoto.

Sasha alisema Diamond alisema amevutiwa kuwa mpenzi wake kwa jinsi  anavyofanana na X.girlfriend wake Wema Sepetu.

"Ni kweli nimezaa na Diamond na motto ana miezi mitatu sasa na Diamond ndio alinikatisha masomo yangu.

Friday, September 6, 2013

SNURA:NINA BIFU NA PESA TU.

MSANII maarufu wa filamu na mwimbaji Snura Mushi afunguka kuwa hajawahi kuwa na bifu na Wema wala Shilole zaidi ya kuwa na bifu na utafutaji pesa.

Akizungumza kupitia kipiti cha mitikisiko ya pwani kinachorushwa kupitia radio ya Times FM hivi karibuni Snura alisema hajawahi kuingia kugombana na msanii yeyote kama inavyosemakana bali yeye anafikiria kutafuta pesa zaidi.

Snura alisema Wema ni rafiki yake na hawakuwahi kugombana zaidi ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari ambazo sio za kweli na kuonyesha akuwa kuna ugomvi kati yao.

Mimi sina bifu na msanii yeyote wala haijawahi kutokea kuingia katika malumbano ninachowaza ni kutafuta pesa kwahiyo mimi nina bifu na pesa"Alisema

Snura alisema kwasasa anafikiria kuanza kufanya nyimbo ya pamoja na msanii maarufu wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuph ili kuongeza ladha ya muziki wake. 

Msanii huyo ambaye anatamba na nyimbo yake ya nimevurugwa alisema kwasasa anafanya juhudi za kujitambulisha zaidi ndani ya nchi kabla hajaanza kujitangaza kimataifa.

 

NSHOMA AZIDI KUUTANGAZA MUZIKI WA ASILI NJE YA NCHI.

MWIMBAJI maarufu aliyewahi kushiriki katika mashindano ya Epiq Bongo Star Search Nshoma Nkwabi aahidi kuendelea kuutangaza utamaduni wa Tanzania nje ya nchi kupitia muziki wa asili.

Akizungumza na blog hii hivi karibuni Nshoma alisema kupitia muziki wa asili ambao anafanya ameweza kuitangaza Tanzania katika nchi mbalimbali anazoalikwa kwaajili ya kuimba.

Nshoma alisema kupitia mialiko hiyo kutoka nchi mbalimbali ikiwemo ujerumani,Swizland na Kenya ameweza kutangaza vizuri nchi yake ambapo mbali na kuimba pia nacheza.

"nimekuwa nkipata mialiko mingi kutoka nje ya nchi ambapo mara nyingi nikienda huko naenda kuimba pamoja na kucheza nyimbo mbalimbali za asili"Alisema.

Nshoma alisema mbali na mialiko hiyo sasa hivi yupo katika maandalizi ya maonyesho ya Chicago yanayofanyika Little Theatre  yanayofanyika kila mwaka na anaendelea kufanya muziki wa Live katika maonyesho mbalimbali.

Msanii huyo ambaye alipata nafasi ya tano katika mashindano ya Epiq Bongo Search pia katika anafanya matangazo mbalimbali ikiwemo tangazo la Vodacom na mambo ya urembo.

REQUEST FOR ADVERTING YOUR BUSINESS THROUGH MY BLOG.

Kesheridhiwani blogspot(sayari ya wanawake) was established on January 2013 under management of Namkeshe Ridhiwani as CEO and Founder of this blog.
Since then it has been hottest in publishing various news concerning celebrities,fashion,sports,catering from different parts of the word.
From this short time since it has been started more than 38,000 people  with different age from different nation arround the world are following this blog.
Hence I request you are advertise your business through this fast growing blog which has potential of being visited and folled by large number of people due our quality,latest and reliable news of women.
Also we have mission which is to be best creator in proving education and updating society through reliable news.
And our costs adverstise on our blog is very cheap compared to the other n you will be required pay for 3 month and for more information contact us.
Our attention is to give top priority to make sure you benefict from your business to advertise your business with us and referred to various place and get more customers.

 TANGAZA NASI KATIKA BLOG HII.
kesheridhiwani blogspot(sayari ya wanawake) ni blog inayoandika habari mbalimbali zinazohusu wanawake ziwe ni za kitaifa ama kimataifa.

Blog hii imeanzishwa rasmi January mwaka huu chini ya uongozi wa mwanahabari Keshe Ridhiwani, ambapo kwakipindi hiki kifupi tayari watu zaidi ya 38,000 wa rika na jinsia tofauti wamekuwa wakitembelea kutoka mataifa mablimbali.

Kupitia maelezo hayo mafupi naleta tena ombi kwa wale wote wanaohitaji kutangaza nasi bas wawasiliane na Keshe moja kwa moja kwa namba ambazo zipo juu upane wa kulia.

Kwa bei ni maelewano kati yetu na mteja lakini inahusisha malipo ya kuanzia miezi 3.

Sunday, September 1, 2013

PICHA:RED CARPET UZINDUZI WA FILAMU YA FOOLISH AGE

MSANII BATULI AKIWA RED CARPET
                                
WOLPER

LULU AKIWA NA MKURUGENZI WA

RAY AKIWA NA MASHABIKI WAKE


MONALISA AKIWA NA MAMA YAKE NATASHA

ANNA MANDELA: MWANAMKE MWENYE RASTA NDEFU ZAIDI DUNIANI, NI ZA FUTI 55 TIZAMA PICHA ZAKE HAPA

Mrs Mandela, 47, anashikilia Guinness World Record kwa kuwa na rasta ndefu zaidi duniani zenye urefu wa futi 55.
 
Humchukua siku mbili kuziosha na kuzikausha nywele zake. Mrs Mandela, ana mtoto mwenye miaka 11 aitwaye Zion aliyezaa na mume wake wa pili, anasema nywele zake zimesaidia uhusiano wake na mumewe.
 
Kwa sasa ameolewa na mume wa tatu na asili yake ni Trinidad and Tobago. Alianza kuzitunza nywele hizo miaka 25 iliyopita.