Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA
imetangaza viwango vipya vya nauli za mabasi ya masafa marefu,
daladala katika jiji la Dar es Salaam, nauli za usafiri wa reli ya kati
na bandari.
Viwango hivyo vimetolewa kutokana na SUMATRA kufuatia
maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na makampuni
binafsi nchini kutokana ongezeko la gharama za uendeshaji.
Ahmad
Kilima ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa SUMATRA amesema viwango vipya
vimetolewa baada ya kufuata taratibu za kisheria na utendaji kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao
kuhusu ongezeko la nauli.
Amesema SUMATRA imeongeza viwango vya juu
vya nauli ya daladala kwa wastani wa asilimia 24.46 na mabasi ya masafa
marefu viwango vimeongezwa kwa asilimia 20.3
Pia amesema ili
kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa
huduma ya usafiri, mamlaka imewataka wamiliki wa mabasi kutotumia
wapiga debe katika kuuza tiketi za usafiri na kwamba watakaokaidi hatua
za kisheria zitachukuliwa.
Bwana Kilima amesema katika kufanya
mapitio ya gharama mbalimbali za bandari na bahari kuu mamlaka
imeridhia ongezeko la gharama kwa wastani wa asilimia 34.3 hivyo TPA
wametakiwa kuboresha huduma kwa wateja kwa kuanzisha kitengo cha
huduma kwa wateja .
Hata hivyo ongezeko hilo la nauli limeenda
sanjari na viwango vya nauli kwa usafiri wa abiria wa reli ya kati
ambapo mamlaka imewataka abiria kukata tiketi na kupanda treni
wakionyesha vitambulisho…
Viwango vipya vya nauli vinatarajia
kuanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili 2013 ambapo nauli ya
mwanafunzi itakuwa shilingi 200 na mtu mzima atalipa shilingi 400 kwa
safari za mijini.