Saturday, January 19, 2013

FILAMU ALIYOIGIZA SAJUKI NA WASTARA YAINGIA SOKONI

   Filamu aliyoyoigizwa  na Marehem Sajuki enzi za uhai wake na mke wake Wastara 'Kivuli' leo imeingia rasm sokon.Filamu hiyo iliyotayarishwa na Wajay Film Co na kusambazwa na kampuni ya Steps imewahusisha pia waigizaji Slim Omary na Mohammed Said.

PICHA ZA LADY JAYDEE AKIWA KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO.

Lady JayDee akiwa katika kilele cha mlima kilimanjaro


Lady JayDee na mumewe Captain Gadna wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufika mlima kilimanjaro

SIKU YA MASTAA WA FILAMU TANZANIA YAKARIBIA


 Wasanii wa filamu nchini wanatarajia kufanya tamasha kubwa lililopewa jina la 'siku ya mastaa wa filamu Tanzania'.
  Tamasha hilo litafanyika tarehe 26 mwezi huu wa kwanza kwenye viwanja vya Dar Live jijini Dar es salaam.Lengo ikiwa ni kuchangia ofisi za shirikisho la filamu Tanzania(TAFF) ambapo kutakua na burudani mbalimbali.
   vikundi vitakavyotoa burudani ni pamoja na bendi ya Twanga Pepeta,Tunda man,Shilole,Snura,Kitale,Joti,Mpoki na wengineyo pamoja na wasanii wote wa filamu wanaounda Bongo Movie.

Rais na Mawaziri wanadharau wabunge kuhusu mabadiliko ya mzunguko wa Bajeti

Yaliyojiri na yanayoendelea kujiri ndani ya Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha kuhusu mabadiliko ya mzunguko na mchakato wa bajeti yanaashiria kwamba Rais na Serikali wanadharau mamlaka na madaraka ya Bunge na wabunge.

Aidha, kutokana na umuhimu wa mzunguko na mchakato wa bajeti katika kuwezesha uwajibikaji kwenye mapato na matumizi ya rasilimali za umma; Waziri wa Fedha anatakiwa aweke wazi kwa umma mabadiliko hayo yaliyofanyika ili wananchi na wadau waweze kutoa maoni na Bunge liweze kuyazingatia wakati wa marekebisho ya kanuni za Bunge yanayotarajiwa kufanywa katika mkutano wa kumi wa Bunge.

Wakati Katibu wa Bunge amenukuliwa tarehe 17 Januari 2013 akisema kwamba pendekezo la mabadiliko ya mzunguko na mchakato wa bajeti bado linajadiliwa na kwamba iwapo litaafikiwa, uamuzi utatangazwa mapema mwezi ujao (Februari 2013) wakati wa mkutano wa Bunge; upande wa Rais na Wizara ya Fedha wameshapitisha na kuanza kutekeleza mzunguko na mchakato mpya wa bajeti kuanzia mwezi Disemba 2012.

Kwa upande wangu nitashiriki vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi wiki ijayo ili nipate mwanya wa kumhoji Waziri wa Fedha kwa kurejea matakwa ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Fedha za Umma, Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sheria ya Ununuzi, Sheria ya Ukaguzi na kanuni zinazoongoza mzunguko na mchakato wa bajeti nchini.

Rais na Serikali wamepitisha na kuanza kutekeleza mzunguko na mchakato huo mpya wa bajeti bila kujali kwamba suala hilo; pamoja na kanuni za ndani ya Serikali linatawaliwa zaidi na Kanuni za Kudumu za Bunge (Kanuni ya 77 mpaka 82) ambazo hazijafanyiwa marekebisho mpaka sasa.

Tafsiri ya uamuzi huo wa Rais na Serikali wa kuanza kutekeleza mzunguko na mchakato mpya wa bajeti bila kanuni za Bunge kufanyiwa marekebisho ni kwamba Rais na Serikali wanahakika kwamba marekebisho hayo yatafanyika kama serikali ilivyopitisha kwa upande wake; huku ni kulifanya bunge na wabunge kuwa mihuri ya kupitisha tu yaliyopangwa na Serikali (Rubber Stamps).

Rais akiongoza Baraza la Mawaziri wamepitisha na kuanza kutekeleza uamuzi wa kwamba sasa mipango na bajeti ya nchi itajadiliwa na kuidhinishwa na Bunge ya mwisho wa mwaka wa fedha mwishoni mwa mwezi Juni.

Wizara ya Fedha baada ya kupitishwa kwa uamuzi huo imeshaanza kuutekeleza kabla ya marekebisho ya kanuni na tayari imeshatoa miongozo kwa Wizara, Idara na Mamlaka zinazojitegemea, Sekretariati za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwasilisha makadirio ya bajeti zao mwezi Machi.

Tayari Serikali imeshapanga kwamba Kamati za Kudumu za Kisekta za Bunge zitafanya vikao vya kupitia bajeti mwezi Aprili na hatimaye bajeti za wizara zote kujadiliwa na bajeti ya ujumla kupitishwa ifikapo tarehe 30 Juni 2013; maamuzi hayo yamefanywa na Rais na Baraza la Mawaziri wakati ambapo ratiba za mikutano na vikao vya Bunge hupangwa na Bunge.

Natambua kwamba kwa nyakati mbalimbali wabunge tumetaka marekebisho ya kanuni za Bunge ikiwemo kuhusu mzunguko na mchakato wa bajeti; hata hivyo, Serikali haina madaraka na mamlaka kufanya maamuzi na kuanza kutekeleza mabadiliko hayo bila Bunge kuridhia.

Natoa mwito kwa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wa kiraia kudhibiti hali hii kwa kuwa ushiriki wa kibunge kwenye mzunguko na mchakato wa bajeti kuanzia usimamizi wa maandalizi, upitishaji na ufuatiliaji wa utekelezaji ni suala muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji kwa maendeleo ya nchi.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)
19/01/2013

Friday, January 18, 2013

ODAMA ATOA KALENDA


     Msanii wa filamu Jennifer Kyaka maarufu Odama pamoja na kampuni yake ya J'-Film 4 Life ametoa kalenda ya mwaka 2013 ikiwa ni zawadi kwa wadau wote wa filam za kitanzania.Kampuni inatoa shukran za dhat kwa watu wote waliounga mkono kazi zilizofanyika kwa mwaka 2012.
      Kalenda zote zina picha zake pamoja na wasanii wengine wa wa filamu nchini.

                        HII NI KALENDA YA KWANZA KWENYA KURASA CHACHE TOFAUTITOFAUTI
  


 
                                  NA HII NI KALENDA YA PILI YENYE KURASA MOJA
                           
                                                                 


Thursday, January 17, 2013

UNIQUE SISTERS WAJA NA CLUB BANGER (NEW 2013)

Wasanii wa bongo fleva ambao waliteka soko la muziki mwanzoni wa miaka ya 2000 ambao ni ndugu watatu(Unique sisters)waja na nyimbo yao ya Club Banger ikiwa ni ujio wao mpya.

NYAMA CHOMA YA NG'OMBE NA VIAZI

 
Nyama choma ni chakula kizuri ambacho unaweza kula wakati wa mchana au jion.Unaweza kuandaa chakula hiki katika mlo wako wa leo. ni rahisi kuandaa.

       Mahitaji
Nyama ya ng'ombe  bila kuikata stek(pande kubwa)   1/2 kilo

Viazi vilivyomenywa na kukatwa duara(sles)              4 vikubwa

Kitunguu swaum na tangawizi iliyosagwa                   2  vijiko vya chakula

Pilipili mbichi iliyosagwa                                            1kijiko cha supu

Mtindi (Yoghurt)                                                       1/2 Kikombe cha chai

Pilipili manga ya unga                                              1kijiko vya chai 

Bizari ya pilau ya unga                                            2vijiko vya chai


Chumvi                                                                   kiasi
 
 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.  Changanya kitunguu swaum, tangawizi, chumvi, pilipili manga, pilipili mbichi, mtindi na bizari ya pilau katika kibakuli kidogo.

2.    Ichanje chanje nyama upate kuingiza mchanganyiko huo wa masala, kisha tia kidogo kidogo katika hizo sehemu wazi katika nyama na uroweke pande la nyama kwa muda  wa nusu saa
       
       Andaa jiko la mkaa liwe na moto kias weka wavu unaotumika kuchomea au jiko la kuchomea nyama weka nyama na iache kwa muda wa saa1.
 
  3.  Au unaweza kutumia oven,liweke katika trea ya kupikia ndani ya jiko (oven). Ifunike kwa jaribosi ya kupikia (foil paper) na ipike katika moto mkali 400º- 450º kwa muda wa saa1.

4.    Karibu na kuwiva, vitie viazi chumvi na pilipili manga kidogo na  umwagie juu ya nyama na uendelee kupika hadi viazi viwive pia.

5.    Epua ikiwa tayari kuliwa.Chakula hiki unaweza kula na mikate,salad au aina yeyote ya juisi au kinywaji ukipendacho.



 

  

 

Wednesday, January 16, 2013

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AWAFANYIA SHERRY PARTY WENZA WA MABALOZI JIJINI DAR

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha wake wa mabalozi nchini kwa mwaka mpya2013,hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini dar es salaam jana. 
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(mwenye kilemba kushoto)akipongezana na consulate wa jamhuri ya Poland Bi.Grazyna Tairo kwenye hafla ya kuwakarbisha wenza wa mabalozi nchini jana,katika viwanja vya ikulu.
Mke wa makau wa Rais Mama Asha Bilal(kushoto)akibadilishana mawazona mkewa waziri mkuu Mama Tunu Pinda(kulia)katika hafla maalum.
<
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(kushoto)akisalimiana na mdau Fauzia Aboud katika hafla hiyo katika viwanja vya ikulu.

Sunday, January 13, 2013

HATUA ZA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO 2013


       Habari za mwaka mpya mfuatiliaji wa blog yangu...hongera kwa kuchaguliwa kuuona mwaka mingine wa 2013,ni jambo la kushuruku na kuongoza juhud zaid katika shughuli zetu za kila siku.

       Wengi tulikuwa na malengo mwaka2012 lakini tulifanikiwa kiasi gani? kwanini haikuwa kwa 100%? kikwazo ni nini? inawezekana hukujua njia sahihi yakupita au wewe ulikuwa adui wa ndoto zako.

     Leo tuangalie hatua sahihi zakutuwezesha kufikia malengo au ndoto zetu tulizonazo.
Anza na moja;
    Unaweza kuwa na ndoto nyingi ambazo unatamani zikamilike mwaka huu lakini ni vizuri aanze na moja,hii itakusaidia kufikiria zaidi na kufanikiwa kwa urahisi.
Amini utafikia malengo;
    Adui wa kwanza wa ndoto zako unaweza kuwa wewe mwenyewe kwa unajipuuza au kujikatisha tamaa katika lile ambalo umeamua kufanya.amini wazo lako ni zuri na ni kubwa .
Omba ushaur;
    Unachotaka kufanya chochote lazima kuna watu ambao tayari wamefanya na wamefanikiwa,hivo ni vizuri kuomba ushauri kwao ili iwe rahisi kujua njia yakupita.Usiogope kuonekana hufahamu ni njia nzuri yakujifunza.
Badilisha mfumo wa maisha;
     Inawezekana ukawa na matumizi mabaya au huna mpangilio mzuri wa pesa zako.sasa ni wakat wakubadilika na kuanza kujinyima vitu ambavyo si vya lazima ili kuweka akiba.Hii itakusaidia kuwa na matumizi mazuri hasa kwa wenye ndoto za biashara.
Weka muda wakutimiza malengo;
     Mfano; unahitaji kufungua biashara weka akiba kwa muda sahihi.Panga kama ni miezi mitatu au sita ikiisha niwe nimetimiza kiasi fulani kwaajili ya kuanza kutimiza ndoto yangu.
Waambie wengine kuhusu malengo yako;
      wapo watu waliokuzidi umri,unaowaamini,kaa nao waambie kile unachofikiria kufanya waeleze kwa kina.Wanaweza kuwa wazazi.mke,mume au ndugu hata rafiki unaweza kupata jambo jipya kutoka kwao katika kuboresha ndoto zako.
Kua mgumu kukata tamaa;
       Muda uliotegemea kutimika ndoto yako umepita na hujakamilisha,usikate tamaa jipe moyo jipange upya fikiria wap ulikosea.
 Mtegemee mungu;
     Zote nilizokuelezea ni njia lakini mtegemee mungu,muombe katika yote ambayo unataka yatimie mana bila yeye hata 2013 tusingeweza kufikia.tchaoo