Saturday, March 23, 2013

MICHAEL JORDAN ADAIWA KUKWEPA MAJUKUMU

 



Sakata la Michael Jordan la kudaiwa kukwepa kubeba majukumu
ya kumlea mtoto wake limechukua sura mpya baada ya mama
 wa mtoto huyu, Pamela Smith kupeleka maombi maalum kwa Jaji
 wa kesi hii kumtaka atoe amri ya kufanya vipimo vya DNA kati
 ya Jordan na mtoto wake.
Hatua hii imekuja baada ya Jordan kukataa kuwahi kumlea
 mtoto huyu ambaye anatambulika kwa jina Grant Taj Reynolds
aliyezaliwa mwaka 1996
.
Katika nyaraka mpya ambazo Pamela Smith ameziwasilisha,
mwanamama huyu ameandika kuwa ana uhakika kuwa
Michael Jordan ndiye baba halisi wa mtoto wake kwa sababu
 hesabu zake zinaonyesha kuwa miezi 9 kamili kabla ya kujifungua
 mtoto wake alilala na nyota huyu wa zamani wa mpira
wa kikapu.
Bado Jaji ajatoa maamuzi mpaka sasa kuhusiana na hatua
 ambayo itaamua hatma ya nyota huyu na familia mpya ambayo
inawezekana kuwa ni ya kwake.


Thursday, March 21, 2013

FILAMU YA MWISHO YA KANUMBA YAZINDULIWA SIKU YA KUMBUKUMBU YAKE YA MWAKA1

 
Kanumba-Movie-ya-mwisho-kabla-ya-kufariki
     Tarehe 7/4/2012 ndiyo siku ambayo marehemu Steven Kanumba alifariki dunia, kwenye kumbukumbu yake mwaka huu kutakuwa na uzinduzi wa filamu ya mpya ya Kanumba titled “Love and Power”.
      Hii ndiyo movie ya mwisho Kabisa ya Kanumba ambayo siku hiyo kutakuwa na misa ya kumuombea kwenye kanisa la Kimara na baada ya hapo mambo yatahamia Leader’s Club. Hapo leaders kutakuwa na uzinduzi wa movie hiyo kwa watu wote ambapo hakutakuwa na kiingilio.

       Seth Bosco ambaye ni mdogo wake Steven Kanumba ameelezea siku hiyo kama ifuatavyo,”Itakuwa ni siku ambayo tutatimiza mwaka mmoja baada ya mpendwa wetu Kanumba kufariki dunia, kumbukumbu yake itaenda pamoja na misa ya kuombea na baadaye uzinduzi wa filamu yake moya inaitwa Power and Love. Watu wote mnakaribishwa kwasababu hakutakuwa na kiingilio chochote siku hiyo”

Wednesday, March 20, 2013

TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS ZAZINDULIWA, KILIMANJARO LAGER YASAINI MKATABA WA UDHAMINI KWA MIAKA MITANO

 


KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2013 LAUNCHED

The Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 was today launched in Dar es Salaam to recognise outstanding achievement in the local music industry over the past year.
       George Kavishe, the Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager said during the launch that Kilimanjaro Premium Lager was proud to stage the event for the 12th time consecutively with the aim of promoting music in Tanzania.
       He said Kilimanjaro Premium Lager is committed to develop the music industry in Tanzania by recognising and awarding Tanzania’s finest music talents. “We want our musicians feel appreciated and recognized for the hard word they are doing and we want Tanzanians to appreciate local music and the contribution made by our musicians towards the economic development of the country”.
        Kilimanjaro Premium Lager is very proud to be associated with these awards and it is hope that this year’s event will be bigger and better.  “We are also proud to announce the extension of our license by BASATA for the next five years.
        The signing of a new contract is a testimony that Kilimanjaro Premium Lager is truly committed to developing the Tanzania music industry as this will take us until 2018

INFO USIZOZIJUA KUHUSU SHOW YA KWANZA YA PREZZO NDANI YA MAISHA

 

Msanii kutoka 254 CMB Prezzo, anatarajia kufanya makamuzi ndani ya New Maisha Club - Dar es Salaam. Show hiyo inatarajia kufanyika ijumaa tar. 5 April 2013.
        Prezzo atakuwa pamoja na wasanii wa hapa nyumbani watakao panda nae stage moja akiwemo Feza, Stereo, Shosteez na wengine surprise kwa mashabaki wa muziki wa kizazi kipya. 

Hii ni mara ya kwanza kwa Prezzo kukamua ndani ya Club.
Na ni msanii ambaye anafanya vizuri katika game, ladha fresh za single zake 2 mpya alizoziachia hivi karibuni akiwa moja ame - dedicate kwa marehemu mchumba wake Goldie ambayo inaitwa "Naija Girl".  na nyingine ni Liqher ambao imekuwa gumzo Afrika Mashariki na Kati, zitasikika kwa mara ya kwanza live siku hiyo

Prezzo siku hadi siku anajizolea umaarufu mkubwa sana bara la Afrika hasa baada  ya ushiriki wake katika jumba la Big Brother Star Game 2012 na kuibuka kinara namba 2 na kutuwakilisha Afrika Mashariki.Msanii ambaye amekuwa gumzo na stori kwa mashabiki mbalimbali ambaye juu ya muonekano wake kuwa wa kipekee (swagga) . Na siku zote amekuwa mtu wa watu.

Prezzo amefanya kazi kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo AY kutoka Tanzania, Wyre, Bamboo, Naziz na wengine kibao. Na nyimbo zake kushika chat katika vyombo mbalimbali vya habari,nyimbo kama Ma Fans, Naleta Action, Ma City Ma Town, Tupendane, For Sure For Shizzle na nyinginezo.

Basi kwa mashabaki wa Prezzo atakuwepo  Liveeeee in Dar...Dont miss out

TAARIFA ZA KMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

 

tff_LOGO1
SERIKALI YARIDHIA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF
Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.
“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.
Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.
Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.
Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.
Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa.

RAIS TENGA AIPONGEZA AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao 2-1 ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Mechi hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jijini Monrovia, matokeo ambayo yanaweka Azam katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano utakaofanyika wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Amesema Azam imefanya jambo kubwa, kwani kushinda ugenini hasa katika nchi za Afrika Magharibi si jambo dogo, hivyo Watanzania waendelee kuiunga mkono na anaitakia kila la kheri katika mashindano hayo.
MSAFARA WA MOROCCO KUTUA NCHINI IJUMAA
Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.
Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.
Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.
Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.
Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana.