Friday, September 27, 2013

PEEPLES...HII NDIO MOVIE AMBAYO WIMBO WA SAIDA KALORI CHAMBUA KAMA KARANGA UMETUMIKA.

Wengi tulioangalia movie hii ya Marekani tumejiuliza wimbo wa Saida Kalori umewafikiaje.Maana ukiangalia movie hii mwanzoni mwanzoni kabisa wimbo chambua kama karanga unasikika na anaonekana mama akiucheza kama sehemu ya mazoezi.
Saida Kalori  hakua akijua chochote kuhusu nyimbo yake kutumika katika movie hiyo.Pia aliyewahi kuwa manager na producer wa Saida hakuwa akijua chochote zaidi ya kupigiwa simu kutoka Marekani na wanawe waliyoiona movie hiyo. 


Zifuatazo ni baadhi ya picha za movie hiyo







Chanzo:Dina marios, blogspot
 

Thursday, September 26, 2013

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUPAKA MAKE'UP

Vipodozi au Makeups ni urembo unaopendwa zaidi na wanawake wengi, dhamira yao ikiwa ni kubadili muonekano wao uliozoeleka ili wapendeze.

Mara nyingi watu wanapopaka makeups tofauti hujitokeza usoni kutokana na kipodozi hicho kufanya kazi ya kung'arisha na kupendezesha uso.

Unapofika wakati wa kupaka makeups,kwanza unapaswa kuchagua ni ipi itakufaa na kukupendeza. swali la kam kipi kitafaa zaidi kati ya poda au cream,hilo linabaki kwa mhusika kwa kuwa kila mmoja anapendekezo lake,kutokana namna anavyopata matokeo mazuri.


MAMBO YAKUZINGATIA KABLA YA KUPAKA MAKEUPS.

Kwanza jaribu kutafuta make ups inayoendana na ngozi yako na rangi ya mwili wako.

Watu wenye ngozi za mafuta wanashauriwa  kupaka makeup ya poda au unga unga kwani ya cream inaweza kuziba vitundu vya hewa katika ngozi ya uso.

Kwa walio na ngozi kavu wafahamu kuwa, make up ya cream haina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu katika ngozi hivyo kama unahitaji kuwa nayo kwa muda unaozidi masaa nane unapaswa kupaka makeup ya poda iliyozoeleka na wengi.

Hakikisha unapaka makeup kwa kutumia brash zake maalum na si kitambaa au mikono.

Wednesday, September 25, 2013

WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2013 WAPAGAWA NA TAARIFA YA JKT!

  HALI ya sintofahamu imewakumba wahitimu wa kidato cha sita nchini, na kuibua malalamiko miongoni mwa wahitmu hao, kufuatia taarifa iliyochapishwa na mtandao wa Jeshi la Kujenga Taifa 'JKT', ikiwataka wahitimu hao kwa ajili ya awamu ya tatu ya mafunzo maalumu, ikiwa ni mwendelezo wa program maalum ya kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wanafunzi wote wanaohitimu kidato cha sita nchini, kabla ya kujiunga na masomo yao ya elimu ya juu.

              

Taarifa hiyo, ilitanabaisha kuwa ni wito kwa ajili ya awamu ya tatu ya mafunzo hayo, ambapo wametakiwa kuwasili katika kambi walizopangiwa mnamo tarehe 28 septemba mwaka huu, ikiwa imetanguliwa na awamu ya kwanza na ya pili, zilizofanyika mapema mwezi March na June mwaka huu.



Punde tu baada ya kuwekwa kwa agizo hilo, Wahitimu wengi walionyesha kushangazwa na taarifa hiyo, ambapo walihoji ni utaratibu gani unaotumika wa kushtukiza ilihali tayari tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imeshatoa chaguzi za wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali na wapo ambao wamesharipoti kwenye vyuo hivyo.

Huku wakionesha wazi kuchanganywa na taarifa hiyo, baadhi ya wahitimu wameelezea kukerwa kwao na uchachafishaji huu uliofanywa na vyombo hivi vikubwa nchini, na kuhoji ni upi ushirikiano baina ya Tume ya vyuo Vikuu na Jeshi la Kujenga Taifa kituendaji.

Hata hivyo, wapo pia waliodai kuwa pengine taarifa hiyo ilichapishwa bila kukusudiwa kutokana na makosa ya kiufundi (technical errors), Hivyo kuwataka wahusika kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo haraka, Jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika hivyo hali ya sintofahamu kuendelea kutamalaki!
                                         
Mtandao huu ulifanikiwa kutembelea mtandao huo (www.jkt.go.tz), na kushuhudia taarifa hiyo ambayo imedaiwa kuchanganya vichwa vya wanafunzi hao, Huku wengi wao wakijiuliza, waende wapi, Kambini au Vyuoni?????

HAFSA KAZINJA AMUENZI MZEE MUHIDINI GURUMO.

MALKIA wa Zouk Tanzania Hafsa Kazinja aachia nyimbo ijulikanayo kama  “NIMUOKOE NANI” ikiwa ni moja ya njia ya kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa 1960.

Kazinja  ambaye ameibuka upya baada ya kimya cha muda mrefu katika fani hiyo  akiwa na ingizo lake la kwanza kati  ya kumi alizoziandaa kwa kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI” ambao anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.

“Nimeamua kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili  kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa wimbo wake wa “PRESHA” aliomshirikisha Banana Zorro.

Hafsa alisema  ukimya wake umetokana na kufanya utafiti na kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki na akipata mawaidha kutoka kwa wanamuziki nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo, Omar Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na kufanya naye kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni

Kazinja alisema ataitambulisha rasmi ngoma ya “NIMUOKOE NANI” katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa kufanyika OKtoba 1, 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye tamasha hilo nami naahidi kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo wasikose kuja kujionea wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake pamoja na ya ngoma zake zingine mpya"alisema.

Kazinja alisema nyimbo hiyo “NIMUOKOE NANI” ameiandaa katika studio za OM Productions ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul Salvador na Omari Mkali.

Pia Kazinja alisema alifurahishwa baada ya kupata baraka zote za kuuimba nyimbo hiyo kutoka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.