Thursday, July 18, 2013

RAY C AWA KIBONGE

 

Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka.


Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake.

Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka.

UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.

Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga.

Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.

Ray C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza zenyewe.

HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.


Kwa mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia kimatibabu.

Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa , alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.

Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu

RAYUU:SIKO TAYARI KUFANYA DHAMBI KWENYE MWEZI MTUKUFU.

Muigizaji wa filamu Rayuu amesema kuwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani anapenda kumcha mungu na hapendi kufanya dhambi kabisa licha ya watu wachache kutaka aonekane mbaya mbele ya jamii.

  Akichonga na Swahiliworldplanet alisema "Mh... Cpendi kufanya dhambi kabisaaa ndo maana mwezi wote najitahidi kuwa msafi na kumcha mungu. Msafi kimatendo ingawa siku zote matendo yangu ni masafi bali tuh wachache ndo hunifanya nionekana mbaya"

LULU AKABIDHIWA RASMI TUZO YAKE YA MUIGIZAJI BORA WA KIKE 2012-2013 KUTOKA ZIFF(PHOTOS)

    Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni actress maarufu Swahiliwood amekabidhiwa rasmi tuzo yake ya best actress in Swahili movies kutoka Zanzibar international film festival ambayo alishinda hivi karibuni. Ukiachilia tuzo hiyo Lulu pia alipewa kiasi cha pesa ingawa hatukuweza kujua ni kiasi gani ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa washindi wa tuzo hizo kama anavyoonekana pichani hapo chini.

Hongera Lulu na kwa washindi wote wa ZIFF. angalia picha.........................