Thursday, August 15, 2013

UTABIRI WA THEA HATIMAYE WATOKEA KWELI.

Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Ndumbagwe Misayo(Thea) amesema kuwa ule msimu wa ma-miss kuvuma kwenye tasnia ya filamu umeshapita na waliokuwa wakitamba miaka michache iliyopita kwasasa hawasikiki tena au ni majina tu yamebaki lakini katika filamu hawaonekani tena.

 Miaka michache iliyopita Thea ambaye ni mmoja wa waigizaji wenye vipaji vya hali ya juu aliwahi kusema kuwa tasnia ya filamu imevamiwa na mamisi ambao wengi wao vipaji hawana.

 Akizungumza na blog ya Swahili world planet Thea aliyetamba na michezo kadhaa Kaole na sasa katika filamu alisema "Utabiri wangu unafanya kazi kwa sababu kwa sasa wale wasanii walioibukia kwenye mashindano ya u-miss wengi hawasikiki tena.

Wasanii wanatakiwa kutambua kuwa sanaa hii siyo lelemama yaani mpaka kufikia hapa tulipo tulifanya kazi ya ziada, tulisota sana kwenye vikundi"
Kwasasa Thea yupo location akishuti filamu mpya akiwa na Jacob Stephen(JB), Shamsa Ford na Bi. Hindu

LULU NA WASTARA WAKUTANISHA PAMOJA


Waigizaji maarufu wa filamu nchini Elizabeth Michael(Lulu) na Wastara Juma wana mpango wa kucheza filamu pamoja
 
 
Wawili hao pia wameonekana katika picha za pamoja hivi karibuni na mashabiki wao kudhani kuwa wanakuja pamoja kikazi.
Tutokana na kuonekana huko pamoja mashabiki wao wanadhani wanaweza kushirikiana na kutoa muvi kali iwapo itakuwa kweli.

Mpaka wakati hatujapata uhakika kutoka kwao wenyewe kuwa ni kweli au ni uzushi tu.

 

EFRANCYAH AGEUKIA MUZIKI

Efrancyah Mangii ambaye ni muigizaji wa filamu ameamua pia kuingia katika muziki wa Bongofleva akitarajia kuimba mahadhi ya Afro pop.

Akizungumza na blog hii Efrancyah alisema kuwa kwasasa yupo katika mazoezi makali na wiki ijayo anatarajia kuingia studio.

Aliongeza kwa kusema kuwa atamshirikisha mwanamuziki mwingine lakini hakuwa tayari kuweka jina la msanii atakayemshirikisha kwa wakati huu.

Kuingia kwa Efrancyah kwenye tasnia ya muziki kunazidi kuongeza idadi ya wasanii wa filamu waliojitosa katika muziki pia kama vile Shilole, Aunt Ezekiel, Snura Mushi, Kingwendu, Bambo, Mzee Magari, na pia Wema Sepetu yupo mbioni kuachia wimbo wake.

Tuesday, August 13, 2013

NAFASI YA WANJA KATIKA UREMBO.

Wanja ni miongoni mwa vipodozi muhimu kwa wanawake.Ukiondoa mafuta na rangi ya mdomo,mara nyingi wanja umekua ukichukua nafasi katika kukamilisha shughuli zima yakujpodoa.

Licha yakutumia wanawake,wanja pia umekua ukitumiwa na wanaume wakilenga kuboresha muonekano wa macho yao.
Kwa kawaida,kila mmoja anajinsi yake yakutumia kipodozi hiki muhimu.

Lisha yaukweli huo mara nyingi watumiaji wamekua wakipata matokeo wasio yatarajia.
Hiyo inatokana nakutokujua namna hasa yaupakaji wake.kupitia makala haya leo utapata uelewa kuhusu namna bora yakutumia urembo huo.

AINA YA WANJA
Zipo aina tatu za wanja ;ambazo ni wanja wa maji,kalamu.wa kidole na poda, huku kila moja ukiwa na matumizi yake.
   Kuna kanuni maalumu katika upakaji wa wanja kwenye macho,ambapo warembo wengi wamekuwa hawazingatii.
   




FLAVIANA MATATA AINGIA KWENYE ORODHA YA WANAMITINDO SABA WENYE KIPATO ZAIDI


NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.

Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na  wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.

Mbali ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.

Flaviana Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake aliendelea na fani ya  uanamitindo Afrika kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models.

Akizungumza kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na nchi yangu”.
 

Monday, August 12, 2013

SHAMSA: DINI HAIWEZI KUNIKOSESHA NDOA


Mwigizaji wa filamu maarufu Shamsa Ford 'Shamsa' akiri kuwa mpaka sasa hajajua ndoa yake itafungwa katika maadili ya dini ipi kutokana na kutofauti iliyopo.

Akizungumza na blog hii hivi karibuni Shamsa alisema ingawa vikao vya harusi tayari vimeanza lakini bado yeye na mchumna wake hawajajua kuhusu ndoa yao itafungwa kwa iman gan.
Shamsa alisema yeye ni muislamu na mumewe mtarajiwa Dickson ni Mkirsto lakini wanaamini tofauti hiyo haiwezi kukwamisha ndoa yao kwani wote wanaamini mungu ni mmoja.

"Mimi na Dickson kweli tupo katika dini tofauti lakini hiyo haiwezi kukwamisha lengo letu kwani mungu ni mmoja na ni jambo lakukubaliana mimi kumfuata au yeye kuja katika dini yangu"Alisema Shamsa.

Pia mwigizaji huyo alisema katika kuonyesha upendo kwake mchumba wake alifunga katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa ramadhani.


Shamsa aliongeza kuwa ndoa ni japo muhimu kwao kwa sasa pamoja na mtoto wa kike aitwaye Teddy ambaye anahitaji mapenzi ya baba na mama.

Ndoa hiyo ya imekuwa ikitajwa kuwepo na kuahirishwa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya Shamsa kutokua tayari kuolewa lakini sasa wameamua kufanya kweli.