Wednesday, July 10, 2013

AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA S.AFRIKA

HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..


 
 

Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
 
               Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

           Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

            Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

          Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
             hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
              Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.                
              Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.           Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.


Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.



Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.



Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.



Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani

RECHO:SIJIPUNGUZI ILI NIOLEWE

MSANII anaye fanya tasnia ya filamu
nchini Recho Haule amefunguka kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa sasa ili kuimarisha mwili na si kwamba anapunguza uzito ili aolewe kama baadhi ya watu wanavyodai.


Nyota huyo mefunguka hivyo baada ya kuibuka tetesi zilizotufikia katika blog hii kutoka kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo ya filamu.

"Kwa sasa nafanya mazoezi kwaajili
ya kutunza hali ya afya yangu,nimekuwa
nikifanya mazoezi  ilikuutunza
mwili wangu uwe katika hali ya afya
njema,"alisema Recho .


 

Monday, July 8, 2013

PENNY AKIWA NA MKWEWE MAMA DIAMOND SIKU YA BIRTHDAY.

Penny alikiwa na mama mzazi wa msanii Naseeb Abdul katika siku ya kuzaliwa kwa mama huyo. 
Zifuatazo ni baadhi ya picha za siku ya birthday.
Penny na Mama Diamon wakilishana keki

Penny akimlisha keki Mama Mkwe

Keki pamoja na vyakula mbalimbali vilivyokuwepo siku hiyo

watu mbalimbali waliohudhuria

Mama Diamon akiwa na dada yake Diamond

Sunday, July 7, 2013

GRACE MACHEL MANDELA MWANAMKE PEKEE ALIYEWAHI KUWA FIRST LADY KWENYE NCHI MBILI

Graca Machel alizaliwa 17 october 1945 Msumbiji katika utawala wa mreno eneo la gaza.Graca mnamo tarehe 11 november 1975 aliolewa na mpigania uhuru wa msumbiji na rais wa kwanza wa msumbiji Somora Machel.


Kabla ya kuwa mke wa rais Graca Machel amewahi kuwa mwalimu na pia katika uongozi wa mumewe Somara Machel aliweza kuwa waziri wa elimu na kilimo nchini Msumbiji.Somora na Graca walifanikiwa kupata watoto wawili Josina Machel na Malengani Machel.Mnamo mwaka 1986 Graca alibaki mjane baada ya mumewe na rais wa zambia wa kwanza Somora Machel kupata ajari ya ndege na kupoteza maisha.

                              akiwa na mume wake wa kwanza.

Tarehe 18 july 1998 aliolewa kwa mara ya pili na rafiki wa mumewe kipenzi na rais wa afrika ya kusini mzee Nelson Mandela na kuwa mke wa Tatu wa nelson mandela.Amekuwa mke wa rais kuanzia mwaka 1998 mpaka 1990 mandela alipoachia madaraka mpaka sasa ndo Graca machel ndo mke wa mandela na ndo mwanamke wa kwanza dunian katika historia kuolewa na viongozi wa nchin tofauti barani afrika na mke wa rais mala mbili katika offisi mbili tofauti msumbiji 1975-1986 na afrika ya kusin 1998-1999.

Graca Machel amewahi kuwa mtetezi wa haki za wanawake na watoto ba mnamo mwaka 1997 alipokea British Dame tuzo kwa ajili ya kazi yake iyo.
Akiwa na Nelson Mandela.

HATIMAYE NATASHA AOLEWA

Hatimaye Mwigizaji wa siku nyingi Natasha ambaye ni mama mzazi wa Monalisa amefunga ndoa baada ya kufanya sherehe mbalimbali zakushindikiza harusi hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.
 
Pongezi nyingi kwake kwakuweza kufanikisha ndoa yao na mungu awaongoze.

DIDA AOLEWA KWA MARA YA TATU

                              Mtangazaji wa Times FM Dida Shaibu akiwa na   mumewe Ezden Jumanne ambaye pia ni mtangazaji wa Times siku ya ndoa yao ambayo ilifanyika siku ya Ijumaa.
                          Mtangazaji Penny aliwa na na Bib harusi Dida
                                          Dida akiwa katika pozi