Sunday, September 8, 2013

HUYO NDIYE MWANAMKE ALIYEWEKA RECORD YA DUNIA ya KUWA NA MIGUU MIREFU KUPITILIZA.

Ama kweli ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni" Katika hali isiyokuwa ya kwaida huyu ndiye mwanamke aliyefanikiwa kuingiza katika kitabu cha kumbukumbu ya Dunia WORLD RECORD GUINESS BOOK. La kushangaza zaidi walimkutanisha na mtu mfupi zaidi Duniani.




NAMNA YA KUANDAA KEKI YA TENDE.

Unga                                   3 kikombe

Baking powder                   3 Vijiko vya chai

Sukari                                 ½ Kikombe
Tende iliyokatwa ndogo ndogo   2 vikombe

Maji yamoto                                 2 vikombe
Siagi                         4 Vijiko vya supu (au vikombe 2 vya kahawa)

Mayai                           2
Cream                              vikombe 2 Vya Kahawa

Tangawizi ya powder         2 Vijiko vya chai

Kungu manga                          1 kijiko cha chai

Mdalasini                                  1  kijiko cha chai

Hiliki                                         ½  kijiko cha chai

Vanilla                                       4  vijiko vya chai

 Vipimo Vya Karamel

Sukari ya buni (brown sugar) 5 Vijiko vya supu

Siagi                                        6 Vijiko vya supu
Lozi zilizomenywa na kukatwa
Nyembamba                                        1 kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1)   Tia maji ya moto katika tende kuiroweka kidogo.

2)   Changanya unga na baking powder vizuri katika bakuli.

3)   Tia vitu vyote vingine na uchanganye vizuri.

4)   Mimina katika bati la duara la kupikia keki ulilolipaka siagi kidogo.
    
5)   Ipikie (bake) katika moto  wa 300° kwa muda wa kama saa.

6)   Iweke katika sahani au bakuli la keki na mwagia karamel juu yake, kisha haraka upambie lozi.

 Namna ya kutayarisha Karamel
Yayusha siagi katika sufuria ndogo au frying pan kisha tia sukari ya brown.

Inapoyayuka, mwagia katika keki.