Saturday, June 8, 2013

NYOKA AITWAE MATILDA AGUNDULIKA TANZANIA.


Nyoka aina mpya duniani mwenye magamba ya njano na nyeusi na macho ya kijani nyepesi, na mapembe mawili amegunduliwa huko Tanzania.


Na amepewa jina la mtoto wa miaka 7 aitwaye Matilda.

Matilda aligunduliwa nchini Tanzania maeneo ya kusini magharibi miaka miwili iliyopita na alitambulishwa mwezi uliopita kama aina mpya ya nyoka iliyojulikana katika jarida la Zootaxa.

Tim Davernport mkurugenzi wa shirika la hifadhi ya wanyama pori Tanzania alikuwa ni mmoja katika timu ya watu watatu waliomgundua nyoka huyo.

Nyioka huyo alipewa jina la mwanae Matilda mwenye umri wa miaka 5 kwasababu alikuwa akimpenda sana nyoka huyo na kumwangalia saa zote.

Katika miongo mitatu iliyopita ni aina za nyoka watatu tu waliogundulia katika bara zima la Afrika na kuanya utambuzi huo kuwa muhimu na wa nadra sana.

Shirika la wanayampori halisemi ni wapi hasa alikopatikana nyoka huyo ili kuzuia wawindaji wanaotafuta fedha . 

Imeandaliwa na:Christina Mokmirya 

BIKINI ZAPIGWA STOP MISS WORLD


Bikini ni vazi lililozoeleka kuvaliwa katika mashindano ya urembo likiwa vazi la ufukweni lakini tofauti na miaka yote mwaka huu waandaaji shindano la mrembo wa dunia wamesema  vazi hilo halitatumika kwenye shindani la hilo.

Wakieleza sababu za kutokutumika kwa vazi hilo ni taratibu za kimaadili kwa vile shindano hilo linafanyika kwa mara ya kwanza mashariki ya mbali katika nchi ya indonesia ambapo 90% ni waislamu.

Walisema badala yake warembo wote 137 watavaa vazi kuogelea la utamaduni ili kupunguza mtazamo tofauti wa kimadili kuhusu shindano  hilo.

Kwanza mara ya kwanza indonesia inakuwa mwenyeji wa shindano litakalofanyika baadaye september mwaka huuu

(source:the sun).

Thursday, June 6, 2013

MPIGIE KURA FEZA ABAKI KWENYE BIG BROTHER


Je leo umempigia kura Feza ili aweze kubaki kwenye jumba? kama bado Andika neno Feza kwenda 15456 au kupitia http://bigbrotherafrica.dstv.com/vote/

Tuesday, June 4, 2013

WANAUME SOMENI HAPA FAIDA ZAKUPIGWA VIZINGA NA WAREMBO

Vijana wengi tumekuwa tukilalamika kwamba mabinti wa siku hizi wana mizinga ya reja reja ten mikubwa.

Hili jambo ukiliangalizia katika “big screen” ni jambo ambalo linakufanya utafute hela if you really want to be with a girl of your dreams though sio lazima a girl of your dreams awe mpiga mizinga!!!!!
Jambo hili zuri nahisi vijana wengi hatujaligundua na badala yake tunalichukulia in a negative way na kubakia tunawalalamikia hawa mabinti, ila kumbe katika hali halisi wanatusaidia.
Maana katika hali ya kawaida lets say kama umeajiriwa somewhere, mshahara peke yake hautoshi kumkeep huyo binti unayemuita wa kisasa au wa mizinga! Sasa kulingana na mahitaji yake kuwa makubwa lazima utatafuta njia nyingine za kupata hela tuseme labda utawekeza mahali.

Lengo likiwa kuhimili mizinga ya huyo binti na kuendelea kumuweka karibu, ila mwisho wa siku unajikuta katika kuwekeza kwako una make faida zaidi ya hizo demands na kwa maana hiyo unakuwa na salio ambalo unaweza kujifanyia maendeleo yako mengine.
Ila kama huyo binti asingekuwa na hizo demands kubwa ungeridhika na mshahara wako, maana utakuwa unawatosha na mwisho wa siku hata kuwekeza mahali huwezi fikiria , na maendeleo yako bila shaka yatakuwa si sawa na yule anayemmiliki binti wa kisasa!!!!!!!!!!

Nahitimisha kwa kuwatia moyo mabinti wa kisasa waendelee na moyo wao huo huo wa kupiga mizinga tena mikubwa ili tutoke hapa tulipo kama Taifa!