Saturday, June 8, 2013

NYOKA AITWAE MATILDA AGUNDULIKA TANZANIA.


Nyoka aina mpya duniani mwenye magamba ya njano na nyeusi na macho ya kijani nyepesi, na mapembe mawili amegunduliwa huko Tanzania.


Na amepewa jina la mtoto wa miaka 7 aitwaye Matilda.

Matilda aligunduliwa nchini Tanzania maeneo ya kusini magharibi miaka miwili iliyopita na alitambulishwa mwezi uliopita kama aina mpya ya nyoka iliyojulikana katika jarida la Zootaxa.

Tim Davernport mkurugenzi wa shirika la hifadhi ya wanyama pori Tanzania alikuwa ni mmoja katika timu ya watu watatu waliomgundua nyoka huyo.

Nyioka huyo alipewa jina la mwanae Matilda mwenye umri wa miaka 5 kwasababu alikuwa akimpenda sana nyoka huyo na kumwangalia saa zote.

Katika miongo mitatu iliyopita ni aina za nyoka watatu tu waliogundulia katika bara zima la Afrika na kuanya utambuzi huo kuwa muhimu na wa nadra sana.

Shirika la wanayampori halisemi ni wapi hasa alikopatikana nyoka huyo ili kuzuia wawindaji wanaotafuta fedha . 

Imeandaliwa na:Christina Mokmirya 

No comments:

Post a Comment