Friday, September 6, 2013

NSHOMA AZIDI KUUTANGAZA MUZIKI WA ASILI NJE YA NCHI.

MWIMBAJI maarufu aliyewahi kushiriki katika mashindano ya Epiq Bongo Star Search Nshoma Nkwabi aahidi kuendelea kuutangaza utamaduni wa Tanzania nje ya nchi kupitia muziki wa asili.

Akizungumza na blog hii hivi karibuni Nshoma alisema kupitia muziki wa asili ambao anafanya ameweza kuitangaza Tanzania katika nchi mbalimbali anazoalikwa kwaajili ya kuimba.

Nshoma alisema kupitia mialiko hiyo kutoka nchi mbalimbali ikiwemo ujerumani,Swizland na Kenya ameweza kutangaza vizuri nchi yake ambapo mbali na kuimba pia nacheza.

"nimekuwa nkipata mialiko mingi kutoka nje ya nchi ambapo mara nyingi nikienda huko naenda kuimba pamoja na kucheza nyimbo mbalimbali za asili"Alisema.

Nshoma alisema mbali na mialiko hiyo sasa hivi yupo katika maandalizi ya maonyesho ya Chicago yanayofanyika Little Theatre  yanayofanyika kila mwaka na anaendelea kufanya muziki wa Live katika maonyesho mbalimbali.

Msanii huyo ambaye alipata nafasi ya tano katika mashindano ya Epiq Bongo Search pia katika anafanya matangazo mbalimbali ikiwemo tangazo la Vodacom na mambo ya urembo.

1 comment:

  1. Merkur 37C Safety Razor Review – Merkur 37C
    The Merkur 37c is an excellent short handled DE safety razor. It is more suitable for both heavy and https://febcasino.com/review/merit-casino/ non-slip hands หารายได้เสริม and filmfileeurope.com is therefore a great goyangfc.com option for experienced https://deccasino.com/review/merit-casino/

    ReplyDelete