Saturday, March 9, 2013

JADEN SMITH NDANI YA DIMBWI LA MAPENZI NA KYLIE KARDASHIAN

 


Ni moja ya stori kwenye headlines sasa hivi kwamba mtoto wa movie Star Will Smith,
 Jaden Smith (14) na mdogo wa Tv Star Kim Kardashian, Kylie Jenner (15) wako
 kwenye uhusiano wa kimapenzi japo wenyewe
hawajathibitisha hilo.US Weekly wameripoti kwamba
 ni uhusiano mpya ambao umeanza baada ya wawili hawa
 kuwa marafiki kwa muda ambapo wamekua wakionekana pamoja sehemu mbalimbali,
 ya hivi karibuni ikiwa ni  Caffe Nero London Uingereza Jaden akiwa amehudhuria
 party ya mshkaji Justine Bieber kutimiza umri wa miaka 19.


LONDON

WOLPER KWA MARA YA KWANZA APIGA PICHA ZA UTUPU

     Hatimaye staa wa filamu za Kibongo mwenye heshima tele, Jacqueline Massawe Wolper amenaswa ‘laivu’ akiwa amepiga picha chafu inayoonesha sehemu kubwa ya nyeti zake.

    Kunaswa kwa picha hiyo, kumevunja heshima ya staa huyo aliyekuwa pekee hajapiga picha ya namna hiyo kati ya mastaa wa k*** wanaotamba katika tasnia ya filamu hapa Bongo.

FASHION MPYA YA RIHANNA YAZINDULIWA..

 


RiRi amezindua Collection yake ya River Island ambapo hizi
 double top jeans ni moja ya bidhaa zake huku moja
ikiuzwa kwa USD 150, Umeonaje huu ubunifu wa kuitengeneza?
 

2FACE AFUNGA NDOA YA KIMILA







Baada ya kufanyika Harusi ya Kimila Jana,Machi 8,Staa Huyu Anategemea kufanya
harusi nyigine Dubai siku kadhaa zijazo....!!

                 hapa ikiwa ni siku chache kabla ya ndoa hiyo.



BEN POL NA RAMA DEE WALALAMIKIA KUIBIWA KAZI ZAO



Wasanii wa kizazi kipya [Bongo Flava] bado wamekuwa wakilalamika kuibiwa mapato kama sio kazi zao bila ruhusa zao.

Mapato hayo ambayo yako katika mfumo wa miito ya simu, yaani caller tunes wameonekana kutokushiriki kwenye mauzo haya na wengine wameonekana kulalamika moja kwa moja kupitia mitandao ya jamii.

Earlier today, msanii anaefanya vizuri sasa na ngoma zake tofauti, akifanya muziki wa RnB, Rama Dee ameandika katika ukurasa wake wa twitter akilalamikia wimbo wake kuuzwa bila ridhaa yake.
Hii inaonesha kutokuwemo kwa makubaliano ya kuuzwa kwa KUWA NA SUBIRA.

Msanii mwingine alieonekana kuwa na matatizo kama haya Ben Pol, msanii mkali wa RnB kutoka Bongo akiwa na credit nyingi kutokanana na kazi zake nzuri.
Ben pia ameonekana leo kulalamikia suala hili hili akionekana kuhuzunika na kuwa na hasira juu ya hili,
Nafikiri hili ni tatizo linalowasumbua wasanii wengi ingawa hawa ni wachache waliolalamika leo, as fans we wanna see these guys win na kutengenza pesa zao kwa jasho wanalolitoa kwa kazi zao.

So far, suala la caller tunes limekuwa na cnflicts na wasanii wengi huku wengi wao wakidai kuwemo lakini bila ya kupata mapene yoyote au kutopata kabisa kutoka huko kwenye makampuni haya.

UHURU KENYATTA NI RAIS MPYA WA KENYA


Tume ya uchaguzi nchini Kenya imemtangaza rasmi bwana Kenyatta kama mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya baada ya kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa
Uhuru Kenyatta ni Rais mpya wa Kenya. 

Tume ya uchaguzi nchini Kenya imemtangaza rasmi bwana Kenyatta kama  mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya baada ya kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa

WASTARA AENDA KUPUMZIKA UARABUNI

 

Wastara Juma
Stara mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya muda mwingi wa mihangaiko ya kuuguza na hata kumpoteza mumewe anahitaji kupumzika na kujenga akili upya, katika kulifanya hilo ameamua kwenda kupumzika Uarabuni kwa ajili ya kutuliza akili na kujipanga upya, amesema kwa sasa anahitaji kupumzika kwa muda.


Wastara Juma

Stara akiwa na mtoto wake.

    “Nina safari wiki ijayo na kwenda Uarabuni kwa ajili ya kupumzika kisha baadae kuangalia nafanyaje kazi katika staili ipi, kwa sasa itakuwa ngumu kuwepo bila kufanya kazi lakini pia familia imeamua niende huko kama ni sehemu ya kunifariji zaidi kutokana na kipindi hiki kigumu,”anasema Stara.
    Lakini mwanadada huyo asiye na makuu ameamua kwenda huko kupmzika kutokana na hali ya filamu ilivyo sasa ambapo watayarishaji wanajikuta wakikikaa kwa muda mrefu wakisotea kazi zao kutoka pasipo na wakati maalum, soko la filamu kwa sasa inasemekana ni gumu kuliko ambavyo jamii inaliona ukiona kazi imetoka sokoni ujue watu wametabika kwa kiwango kikubwa.
.

     Tunamtakia mapumziko mema na safari yenye Baraka na baadae akirudi arudi na nguvu mpya kwa ajili ya kuendeleza sanaa yetu Bongo

MATUKIO BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI KENYA



Wafuasi wa Uhuru Kenyatta walijitokza mapema kusherehekea ushindi wa mgombea wao Uhuru Kenyatta katika eneo bunge la Gatundu


 Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.

Hata hivyo tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano asubuhi saa za Afrika Mashariki
                 


09:23 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu ambayo ndio ngome kuu ya Raila Odinga, Ann Mawathe anasema kuwa wafuasi wa Odinga wamenuna kwa kuwa mgombea wao ameshindwa kwenye uchaguzi lakini wanaendelea na shughuli zao kama kawaida
08:45 Mjini Nyeri moja ya ngome za Uhuru Kenyatta ni vifijo na nderemeo tupu barabarani kusherehekea ushindi wake




08:12 Mjini Nakuru mamia ya watu waliamka asubuhi na mapema kusherehekea barabarani kafuatia taarifa za mgombea wao wa urais Uhuru Kenyatta. Wameonekana wakibeba mabango na matawi kama ishara ya furaha yao
08:06 Josiah Mayaka Wa Kisii Kenya anasema kuwa watu wengi Kisii wamesononeka sana ila kwa sababu limetendeka wamekubali matokeo shingo upande.
07:47 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameimba wimbo wa taifa wakiwa kando ya majengo ya bunge kusherehekea ushindi wa mgombea wao


07:39 Mjini Eldoret ngome ya William Ruto mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta sherehe zimeanza mapema na asubuhi baada ya matokeo kudhihirika wazi kuwa Uhuru Kenyatta ndiye mshindi
07:35 Hanif Mohhamed wa Mombasa-Kenya kupitia facebook naona mustakabali wa Kenya ni giza tupu, saa hii anasema anatafakari njia mubadala ya kukumbana na changa moto zitakazo wapata kama wakenya baada ya athari kuanza kuchimbuka.
07:26 Vifijo na nderemeo pamoja na milio ya honi katika barabara ya Kijabe mjini Nairobi kufuatia ushindi wa Uhuru Kenyatta
       07:08Alex Mulwa anasema kuwa wakenya wamechagua viongozi ambao wataleta maendeleo na kuleta mabadiliko katika nchi yao. Alex ,kwa niaba ya wakenya anaomba ICC isitishe na kusimamisha kesi dhidi ya Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ili kuwapa nafasi kuongoza bila wasiwasi

    06:55 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameanza kujitokeza katika baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi kusherehekea ushindi wake
         06:46 Uhuru Kenyatta ana kura 6,173,433 wakati Raila Odinga 5,340,54. Hii inampa Uhuru ushindi wa asilimia hamsini nukta tatu ambao unahitajika chini ya katiba mpya kwa mtu kushinda uchaguzi wa rais.
       06:40 Tume ya uchaguzi baadaye leo itatangaza mshindi wa uchaguzi ingawa hesabu ya kura inaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kinyang'anyiro.

Friday, March 8, 2013

MAJUTO AONGOZA MSAFARA WA WAIGIZAJI RWANDA

                                                                     King Majuto
Amri Athuman

  KOMEDIANI Mkongwe katika tasnia ya filamu na vichekesho Swahiliwood Amri Athuman ‘King Majuto’, akiongozana na wasanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo, yaani Ray, JB, na Irene Uwoya wapo nchini Rwanda kwa mwariko wa Ishusho Arts ya Rwanda wakiwa ni wageni waarikwa katika utoaji wa tuzo za filamu zilizoandaliwa nchini humo.

JB mwigizaji nyota wa filamu Swahiliwood.


Jacob Stephen
 
King Majuto pamoja na kundi hilo watakuwa moja kati ya watoaji wa tuzo hizo kwa washindi watakaotangazwa kama washindi wa Tuzo zinazojulikana kama Rwanda movie Awards, wasanii waliondoka jijini Dar es salaam siku ya jumatano kwa ajili ya utoaji wa tuzo ambazo zimezidi kujichukulia umaarufu Rwanda na Afrika Mashariki.
“Nimefarijika sana kwa kuteuliwa kuwa mgeni rasmi katika nchi ya jirani zetu wa Rwanda kwa ajili ya zoezi la utoaji wa tuzo ambazo zimepewa heshima kubwa na wanarwanda na Afrika mashariki pia kwetu ni heshima kubwa sana,”anasema King Majuto.
.                      Ray the greatest muigizaji wa swahiliwood

 

                   Irene uwoya msanii wa swahiliwood 
Wasanii hao wakiwa nchini Rwanda wataonana na mke wa nchi hiyo Paul Kagame mama Jeannette Kagame na kubadilishana mawili matatu kisha kurudi nchini Tanzania, pia kampuni ya Steps Entertainment ambayo ndio wasambazaji wakubwa wa filamu Swahiliwood itapata fursa ya kutangaza filamu zake katika tamasha hilo siku ya utoaji wa tuzo.
Tamasha hilo linafanyika siku ya kesho tarehe 9. March. 2013.

Thursday, March 7, 2013

MADAKTARI WA AFRIKA KUSINI WAELEZA MADHARA MAKUBWA ALIYOYAPATA MHARIRI KIBANDA

 

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alitekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya na juzi alasiri alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
        Habari zilizopatikana jana kutoka Afrika Kusini na kuthibitishwa na uongozi wa Tef zinasema madaktari wanaomtibu Kibanda walibaini madhara zaidi ambayo ni pamoja na kukatika kwa mfupa laini (fizi) unaounganisha pua na mdomo pamoja na kulegea kwa meno takriban sita.
      Taarifa ya Tef iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Neville Meena imesema athari hiyo imesababishwa na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumng’oa meno... “Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake.”
      Kuhusu meno, Meena alisema hayo sita yaliyoelezwa kwamba yamelegea ni mbali na yale mawili yaliyong’olewa katika tukio la awali.

KURA ZA RAILA ODINGA ZINAPANDA KWA KASI

RAILA ODINGA
                                                                  UHURU KENYATTA
                                                                  
 Kenyan Presidential OFFICIAL Results (March 07, 2013):

 Mpaka kufikia saa 5:30 kura zilizohesabiwa kwa upande wa Uhuru Kenyatta - TNA: 3,522,127 na Raila Odinga - ODM: 3,299,391....
 Tuendelee kuwaombea Kenya wamalize uchaguzi kwa amani nautulivu..
  Chagua Amani

Wednesday, March 6, 2013

SABABU ZA KUJERUHIWA KWA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ZATAJWA

                          (waziri wa afya na ustawi wa jamii Hussein Mwinyi akimjulia hali)
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bwana Theophil Makunga amesema maelezo ya awali yanaonyesha kuvamiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa hilo kunatokana na sababu za kazi yake ya uandishi wa habari.
      Makunga amesema Bwana Absalom Kibanda amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana na kumjeruhi baadhi ya sehemu ya mwili wake wakati akirejea nyumbani.
      Tukio hili lililotokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya nyumbani kwake mbezi beach jijini Dar Es Salaam linahusishwa na sababu za kitaaluma kama anavifafanua bwana Theofil Makunga…
      Hussein Bashe ni mkurugenzi Mtendaji wa News Habari Corporation ofisi mwajiri wa Kibanda anasema hakuna kifaa cha kazi kilichoibiwa katika tukio hilo na kuwa wanafanya taratibu kumsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
     Miongoni mwa viongozi waliofika kumtembelea ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Hussein Mwinyi amesema serikali imesikitishwa na kitendo hicho.
    Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar Es Salaam Sulemani Kova amesema wanashirikiana na makao makuu ya polisi katika kufanya upelelezi wa tukio hilo.

Tuesday, March 5, 2013

NONINI APATA SHAVU JINGINE IN PRISK

 


          Star wa muziki kutoka Kenya, maarufu kama Nonini "Mgenge True" ambae kwa sasa ni mtangazaji wa kituo cha redio,  1 FM[KE] amechaguliwa kuwa mmoja wa Member Of The Board Of Directors katika chombo kinachojihusisha na kusimamia na kufuatilia haki za wasanii nchini Kenya (PRISK).

       Hivi karibuni, Nonini alitangazwa kuwa yeye ndiye msanii pekee kutoka nchini humo alieingiza kiasi kikubwa cha hela kutokana na muziki wake, baada ya kuchaguliwa kuwakilisha wasanii katika nafasi hiyo alizungumza hivi
      “I wanna take this opportunity to thank all the artist’s who came out for the PRISK (Performing Rights Organisation Of Kenya) Special AGM today and actually voted MgengeTrue into the Board of Directors! Artists should be involved in running copyright bodies because hakuna mtu anaelewa shida za msanii kama msanii! ”.
 
       Pia wengine waliochaguliwa kuwakilisha wasanii katika bodi hiyo ni aliekuwa jaji Tusker Project Fame, Judge Ian.

Monday, March 4, 2013

AT AELEZEA KUHUSU FUJO WAKATI AKIWA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI KENYA



AT

 Msanii kutoka Tanzania anayewakilisha pande za Zanzibar Mwenye mashabiki wengi Mombasa alikuwa kwenye michakato ya Kufanya Video Yake Mpya Weekend iliyopita na Video hii ilibidi ifanyike Mombasa.

Baada ya Shooting ya video hii kukamilika AT Alikuwa tayari kurudi Dar es salaam kwani alikuwa na Show ya Jumapili Ndani Ya Club Bills.

Japokuwa alikuwa na majukumu Dar es salaam, alipata nafasi yakufanya show kwenye jukwa la mmoja ya wagombea wa Ugavana pale Mombasa na Mgombea huyu anakubalika sana Mombasa Ndio maana Ilikuwa Rahisi kwa AT Kukubali kufanya Show yake.


Story kutoka Mombasa zinasema kuwa AT Alipigwa na kushushwa Kwenye Jukwa kabla show hiyo kuisha,

AT kupitia kesheridhiwani.blogspot amesema kuwa story hizi ni za uongo na anakanusha taarifa hizi kabisa na hakuna kitu kama hicho.

  AT Amekaririwa akisema show hiyo imefanyika na kuisha vizuri. Mgombea aliye fanya show yake anakubalika sana na hakuna mtu aliye leta fujo kwenye show hio.

  Pia AT Amesema kilicho mchelewesha Dar es salaam ni kuchelewa kufika Airport ndio ikabidi atumie gari mpaka Tanga na kuonganisha mpaka Dar es salaam

GARI LA MMOJA WA WAGOMBEA LACHOMWA MOTO KENYA

 

Candidate’s car set on fire in attack




PHOTO | TONY KARUMBA Residents gather around the shell of parliamentary candidate Justus Kizito’s car at Lukango in Shihuli, Kakamega, on March 4, 2013.
 

Shinyalu parliamentary seat candidate Justus Kizito’s vehicle was burnt in a violent confrontation with supporters of a rival over allegations of voter bribery.

Mr Kizito’s Range Rover was set ablaze by a rowdy mob at Lukango in Shihuli, Kakamega, on Monday at about 1am.

Mr Kizito, who was accompanied by his driver and two supporters, is said to have been driving from a meeting with his polling agents when they ran into the supporters of the rival candidate.

Pay allowances

The former Shinyalu MP said he had gone to meet the agents to pay their allowances and make arrangements for their travel to polling centres.

But the group of supporters accused the former MP of driving around the constituency at night bribing voters.

In the ensuing confrontation, the rival’s supporters blocked the way and smashed the windscreen and set the vehicle ablaze.

Kakamega police boss Charles Kinyua said Mr Kizito was slightly injured and fled into a nearby bush.

“Mr Kizito is safe and has recorded a statement with police on the attack. His vehicle was completely destroyed,” he said

Sunday, March 3, 2013

IRENE UWOYA NDANI YA LAST CARD

 

iRENNE UWOYA

Irene Uwoya mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
     MWANADADA mwenye mvuto katika tasnia ya filamu Bongo Irene Uwoya amerudi tena kwa kuingia na filamu ya Last Card msanii huyo alikuwa kimya kidogo kwa ajili ya maandalizi ya filamu na sasa ameingia na last card kazi anayoaamini kuwa itafanya vizuri katika soko la filamu kutokana na uzuri wa kazi hiyo kuandaliwa kwa umakini zaidi, Irene Uwoya ni moja kati ya wasanii wa kike wenye wapenzi wengi wa kazi za filamu nchini.

Filamu ya Last Card

Picha ya Filamu Last Card.
Irene uwoya
Irene Uwoya akiwa kajishika tama kwa pozi.
“Ninafungua mwaka kwa bonge la filamu, sitaki kuwaambia kilichopo ndani ya filamu ya Last card bali mtu akibahatika kuiona atasema mwenyewe kuwa kazi hiyo kwa nini imeitwa Last Card, ni kazi bora sana kwangu na wote tulioshiriki katika filamu na naweza kuwahakikishia wapenzi wa kazi zangu kuwa hii ni kiboko si ya kuikosa,”anajitamba Irene.
          Filamu ya Last Card inakutanisha Irene Uwoya na mwigizaji mwenye sifa za filamu za kimahaba nchini Baba Haji na kuifanya filamu kuwa na visa mikasa ya kuvutia zaidi, inasemeka kuwa Baba Haji ndio msanii ndio msanii pekee bingwa wa kuigiza filamu za mahaba Bongo mwenye uwezo wa kubembembeleza na kushawishi, pia katika filamu hiyo unakutana na wakali wengine kama Janeth Sospeter, Omary Barafu na wasanii wakali katika tasnia ya filamu Bongo, filamu hiyo inasambazwa na Steps Entertainment.

KUPUNGUZA UNENE KWA KUTUMIA ASALI NA LIMAU/NDIMU

 



Asali na limau

Diet ya asali na Limau diet inasaidia kupunguza tatizo la uzito mkubwa/unene .
 Obesity ni hali ya mwili unapokuwa unamafuta mengi kupindukia na mafuta hujitokeza katika tishu za mwili, kwenye moyo, mafigo, ini na viungo kama vile nyonga, magoti na vifundoni na hivyo, watu wenye uzito mkubwa pia  ni rahisi kukabiliwa na magonjwa kadhaa kama kisukari, shinikizo la damu, arthritis, ini na nyongo ya kibofu cha mkojo kupata matatizo.

Asali ni njia nzuri ya asili ambayo unaweza kutumia kwa ajili ya Obesity na kupunguza kwa viwango vya cholesterol mwilini. 
Kufunga/Fasting kwa asali na lemon-juisi, chakula alkali, ina manufaa katika matibabu ya Obesity bila kupata hamu ya kula.
Kwa ajili ya tiba hii ya asili, changanya kijiko moja ya asali mbichi (unheated) na vijiko viwili vya maji ya limau au ndimu katika glasi ya joto au maji vuguvugu (si kuchemsha maji!).
Kunywa mchanganyiko huu wa asali na limau/ndimu kila unapoamka asubuhi tumbo likiwa tupu. Pia unatakiwa kunywa mchanganyiko huu mara baada ya mlo kubwa na vyakula vya mafuta, hii inarahisisha kwenye digestion .
Ukiendelea na tiba asili ya kupunguza uzito unatakiwa kuzingatia kanuni kama vile kutengeneza tabia katoka milo unayokula pia kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.