Friday, March 8, 2013

MAJUTO AONGOZA MSAFARA WA WAIGIZAJI RWANDA

                                                                     King Majuto
Amri Athuman

  KOMEDIANI Mkongwe katika tasnia ya filamu na vichekesho Swahiliwood Amri Athuman ‘King Majuto’, akiongozana na wasanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo, yaani Ray, JB, na Irene Uwoya wapo nchini Rwanda kwa mwariko wa Ishusho Arts ya Rwanda wakiwa ni wageni waarikwa katika utoaji wa tuzo za filamu zilizoandaliwa nchini humo.

JB mwigizaji nyota wa filamu Swahiliwood.


Jacob Stephen
 
King Majuto pamoja na kundi hilo watakuwa moja kati ya watoaji wa tuzo hizo kwa washindi watakaotangazwa kama washindi wa Tuzo zinazojulikana kama Rwanda movie Awards, wasanii waliondoka jijini Dar es salaam siku ya jumatano kwa ajili ya utoaji wa tuzo ambazo zimezidi kujichukulia umaarufu Rwanda na Afrika Mashariki.
“Nimefarijika sana kwa kuteuliwa kuwa mgeni rasmi katika nchi ya jirani zetu wa Rwanda kwa ajili ya zoezi la utoaji wa tuzo ambazo zimepewa heshima kubwa na wanarwanda na Afrika mashariki pia kwetu ni heshima kubwa sana,”anasema King Majuto.
.                      Ray the greatest muigizaji wa swahiliwood

 

                   Irene uwoya msanii wa swahiliwood 
Wasanii hao wakiwa nchini Rwanda wataonana na mke wa nchi hiyo Paul Kagame mama Jeannette Kagame na kubadilishana mawili matatu kisha kurudi nchini Tanzania, pia kampuni ya Steps Entertainment ambayo ndio wasambazaji wakubwa wa filamu Swahiliwood itapata fursa ya kutangaza filamu zake katika tamasha hilo siku ya utoaji wa tuzo.
Tamasha hilo linafanyika siku ya kesho tarehe 9. March. 2013.

No comments:

Post a Comment