Monday, March 4, 2013

AT AELEZEA KUHUSU FUJO WAKATI AKIWA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI KENYA



AT

 Msanii kutoka Tanzania anayewakilisha pande za Zanzibar Mwenye mashabiki wengi Mombasa alikuwa kwenye michakato ya Kufanya Video Yake Mpya Weekend iliyopita na Video hii ilibidi ifanyike Mombasa.

Baada ya Shooting ya video hii kukamilika AT Alikuwa tayari kurudi Dar es salaam kwani alikuwa na Show ya Jumapili Ndani Ya Club Bills.

Japokuwa alikuwa na majukumu Dar es salaam, alipata nafasi yakufanya show kwenye jukwa la mmoja ya wagombea wa Ugavana pale Mombasa na Mgombea huyu anakubalika sana Mombasa Ndio maana Ilikuwa Rahisi kwa AT Kukubali kufanya Show yake.


Story kutoka Mombasa zinasema kuwa AT Alipigwa na kushushwa Kwenye Jukwa kabla show hiyo kuisha,

AT kupitia kesheridhiwani.blogspot amesema kuwa story hizi ni za uongo na anakanusha taarifa hizi kabisa na hakuna kitu kama hicho.

  AT Amekaririwa akisema show hiyo imefanyika na kuisha vizuri. Mgombea aliye fanya show yake anakubalika sana na hakuna mtu aliye leta fujo kwenye show hio.

  Pia AT Amesema kilicho mchelewesha Dar es salaam ni kuchelewa kufika Airport ndio ikabidi atumie gari mpaka Tanga na kuonganisha mpaka Dar es salaam

No comments:

Post a Comment