Irene Uwoya mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWANADADA mwenye mvuto katika tasnia ya filamu Bongo Irene Uwoya
amerudi tena kwa kuingia na filamu ya Last Card msanii huyo alikuwa
kimya kidogo kwa ajili ya maandalizi ya filamu na sasa ameingia na last
card kazi anayoaamini kuwa itafanya vizuri katika soko la filamu
kutokana na uzuri wa kazi hiyo kuandaliwa kwa umakini zaidi, Irene Uwoya
ni moja kati ya wasanii wa kike wenye wapenzi wengi wa kazi za filamu
nchini.
Picha ya Filamu Last Card.
Irene Uwoya akiwa kajishika tama kwa pozi.
“Ninafungua mwaka kwa bonge la filamu, sitaki kuwaambia kilichopo
ndani ya filamu ya Last card bali mtu akibahatika kuiona atasema
mwenyewe kuwa kazi hiyo kwa nini imeitwa Last Card, ni kazi bora sana
kwangu na wote tulioshiriki katika filamu na naweza kuwahakikishia
wapenzi wa kazi zangu kuwa hii ni kiboko si ya kuikosa,”anajitamba
Irene.
Filamu ya Last Card inakutanisha Irene Uwoya na mwigizaji mwenye sifa
za filamu za kimahaba nchini Baba Haji na kuifanya filamu kuwa na visa
mikasa ya kuvutia zaidi, inasemeka kuwa Baba Haji ndio msanii ndio
msanii pekee bingwa wa kuigiza filamu za mahaba Bongo mwenye uwezo wa
kubembembeleza na kushawishi, pia katika filamu hiyo unakutana na wakali
wengine kama Janeth Sospeter, Omary Barafu na wasanii wakali katika
tasnia ya filamu Bongo, filamu hiyo inasambazwa na Steps Entertainment.
No comments:
Post a Comment