Saturday, March 9, 2013

MATUKIO BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI KENYA



Wafuasi wa Uhuru Kenyatta walijitokza mapema kusherehekea ushindi wa mgombea wao Uhuru Kenyatta katika eneo bunge la Gatundu


 Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.

Hata hivyo tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano asubuhi saa za Afrika Mashariki
                 


09:23 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu ambayo ndio ngome kuu ya Raila Odinga, Ann Mawathe anasema kuwa wafuasi wa Odinga wamenuna kwa kuwa mgombea wao ameshindwa kwenye uchaguzi lakini wanaendelea na shughuli zao kama kawaida
08:45 Mjini Nyeri moja ya ngome za Uhuru Kenyatta ni vifijo na nderemeo tupu barabarani kusherehekea ushindi wake




08:12 Mjini Nakuru mamia ya watu waliamka asubuhi na mapema kusherehekea barabarani kafuatia taarifa za mgombea wao wa urais Uhuru Kenyatta. Wameonekana wakibeba mabango na matawi kama ishara ya furaha yao
08:06 Josiah Mayaka Wa Kisii Kenya anasema kuwa watu wengi Kisii wamesononeka sana ila kwa sababu limetendeka wamekubali matokeo shingo upande.
07:47 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameimba wimbo wa taifa wakiwa kando ya majengo ya bunge kusherehekea ushindi wa mgombea wao


07:39 Mjini Eldoret ngome ya William Ruto mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta sherehe zimeanza mapema na asubuhi baada ya matokeo kudhihirika wazi kuwa Uhuru Kenyatta ndiye mshindi
07:35 Hanif Mohhamed wa Mombasa-Kenya kupitia facebook naona mustakabali wa Kenya ni giza tupu, saa hii anasema anatafakari njia mubadala ya kukumbana na changa moto zitakazo wapata kama wakenya baada ya athari kuanza kuchimbuka.
07:26 Vifijo na nderemeo pamoja na milio ya honi katika barabara ya Kijabe mjini Nairobi kufuatia ushindi wa Uhuru Kenyatta
       07:08Alex Mulwa anasema kuwa wakenya wamechagua viongozi ambao wataleta maendeleo na kuleta mabadiliko katika nchi yao. Alex ,kwa niaba ya wakenya anaomba ICC isitishe na kusimamisha kesi dhidi ya Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ili kuwapa nafasi kuongoza bila wasiwasi

    06:55 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameanza kujitokeza katika baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi kusherehekea ushindi wake
         06:46 Uhuru Kenyatta ana kura 6,173,433 wakati Raila Odinga 5,340,54. Hii inampa Uhuru ushindi wa asilimia hamsini nukta tatu ambao unahitajika chini ya katiba mpya kwa mtu kushinda uchaguzi wa rais.
       06:40 Tume ya uchaguzi baadaye leo itatangaza mshindi wa uchaguzi ingawa hesabu ya kura inaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kinyang'anyiro.

No comments:

Post a Comment