Friday, June 28, 2013

HUDDAH MBAYA WA DIVA ATUA DAR

HUDDAH
Aliyekua mmoja wa wawakilishi wa Kenya katika BBA
The Chase, mrembo Huddah Monroe (The Boss Lady)
ametua Dar es Salaam, Tanzania ku-host party ya “Mid
Year Bash” siku ya jumamosi tarehe 29/june/2013.
BASH hilo litafanyika ndani ya ELEMENTS
LOUNGE,
 Na limedhaminiwa na Unity Entertainmen, Heinneken,

na Vocacom.....Watu wengi wanajiuliza itakuwaje pale
watakapo kutana na Diva loveness ambae wamekuwa



na beef kwenye mitandao wakimgombea japo amekuwa
akikataa pindi anapohojiwa..Prezzooo...Aka the boy is Mine


                                                                     diva



 

Wednesday, June 26, 2013

FAMILIA BORA YENYE VIPAJI KWA KILA MWANAFAMILIA

Picha hii ikimuonesha muigizaji nguli kwenye tasnia ya movie
nchini marekani Will Smith akiwa na familia yake..


kutoka kushoto ni Jaden Smith(14) ambaye ni muigizaji na muimbaji,  Willow Smith(12)ni muigizaji    Will Smith
mwenyewe(44)ni muimbaji,mchekeshaji na muigizaji    Jada Pinkett Smith(41) ni mama wa familia hii ambaye ni muigizaji na mwana mitindo na       Mtoto
mkubwa wa will Smith kwa Mama Mwingine Trey Smith(21)ni mchezaji wa basketball.




HATIMAYE MUME WA JOYCE KIRIA APATIKANA

HATIMAYE mume wa Joyce Kiria  Mtangazaji wa Eatv kipindi cha wanawake live Bwana Henry Kilewo  aonekana akiwa ameshikiliwa na polisi  akihusishwa na tuhuma za Ugaidi wa kutumia tindikali.
Kilewo anashutumiwa kummwagia tingikali Musa Tesha sept9 mwaka juzi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga.
"Sijui nilichoitiwa nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito,nimewataarifu mawakili wangu kwakuwa chochote kinaweza kutokea na kwa sasa cha msingi watanzania wanaopenda mageuzi waniombee kwa mungu"Alisema Kileo.
Kwa habari zaidi tembelea blog ya michuzi.

KAJALA AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA WEMA

Monday, June 24, 2013

(PICHA)JOYCE KIRIA ALIPOAMUA KUANDAMANA KWAAJILI YAS MUMEWE.

Mtangazaji Joyce Kiria alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) akitaka kujua alipo mumewe na hatima ya mumewe.
Aliyowabeba ni watoto wake.
 
 
 

JOYCE KIRIA AMLILIA MUME WAKE

Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live Joyce Kiria amlilia mumewe ambaye ni mwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo baadaya ya kukamatwa na polisi.
 
Akizungumza na waaandishi wa habari Joyce mwenyw watoto wawili amesema mpaka sasa hajui chochote kinachoendelea kuhusu mumewe na polisi hawataki kumpa ushirikianio.
 
"Hata nikitaka kumpelekea mumewangu chakula nashindwa nimpelekee wapi mana polisi hawataki kuniambia chochote kuhusu mumewangu na mimi nina watoto hawa nitafanya nini jamani"Alisema kwa uchungu Joyce.
 
Imeelezwa chanzo cha kukamatwa kwa Mume wa Joyce ni vurugu za Igunga/Tabora na mumewe kuambiwa kuwa amemmwagia mtu tindikali.

RIYAMA ATOA SIRI YA KUPEWA TUZO NA KAMPUNI YA STEPS INTERTAIMENT

Msanii maarufu wa filamu Riyama Ally 'Riyama' aeleza siri ya kufanya vizuri katika tasnia ya uigizaji na kudumu kwa muda mrefu.
Alipozungumza na SAYARI YA WANAWAKE hivi karibu Riyama alisema kuwa ni juhudi zake binafsi katika uigizaji pamoja na kuheshimu sana kazi yake.

Riyama alisema zipo sababu nyingi lakini yeye binafsi anaipenda sana kazi yake ya uigizaji na akaamua kuwekeza juhudi zaidi ili kuweza kuwaburudisha na kwaelimisha wapenzi wake pindi watakaponunua kazi zake.
"Naipenda kazi yangu ya uigizaji,najiheshimu na nawaheshimu niniaofanya nao kazi pamoja na kuwa na nidhamu ndio vinanifanya nionekana tofauti"Alisema
Mbali na kufanya vizuri katika kazi zake mbalimbali pia amejipatia tuzo ya msanii bora wa kike msaidizi zilizotolewa hivi karibuni kupitia  kampuni ya step intertaiment.
Mwigizaji huyo ambaye hana skendo aliongeza kuwa amefurahi kupata tuzo hiyo na amemuongezea ari ya kuzidi kufanya vizuri katika kazi zake atakazozitoa.
Riyama aliwahi kufanya vizuri katika kazi mbalimbali ikiwemo ya fungu la kukosa na sasa anatamba na Filamu ya The dream aliyoshirikiana na wasanii wengine akiwemo mwimbaji Khadija Kopa.