Monday, June 24, 2013

JOYCE KIRIA AMLILIA MUME WAKE

Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live Joyce Kiria amlilia mumewe ambaye ni mwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo baadaya ya kukamatwa na polisi.
 
Akizungumza na waaandishi wa habari Joyce mwenyw watoto wawili amesema mpaka sasa hajui chochote kinachoendelea kuhusu mumewe na polisi hawataki kumpa ushirikianio.
 
"Hata nikitaka kumpelekea mumewangu chakula nashindwa nimpelekee wapi mana polisi hawataki kuniambia chochote kuhusu mumewangu na mimi nina watoto hawa nitafanya nini jamani"Alisema kwa uchungu Joyce.
 
Imeelezwa chanzo cha kukamatwa kwa Mume wa Joyce ni vurugu za Igunga/Tabora na mumewe kuambiwa kuwa amemmwagia mtu tindikali.

No comments:

Post a Comment