Wednesday, October 16, 2013

ANDAA KUKU WAKUOKWA

Vipimo:

 

*Kuku mzima        1


Tangawizi   na thomu          1 kijiko cha supu

Mtindi                                   3 vijiko vya supu

Rojo la ukwaju                     2 Vijiko vya supu

Pilipili mbichi                      1 kijiko cha supu

Chumvi                             kiasi

Bizari ya jiyrah (cummin poda) 1 kijiko cha chai

Bizari ya dania (coriander poda.1 kijiko cha chai

Paprika                            1 kijiko cha chai

Kungu manga ya unga      1/2 kijiko cha chai

Hiliki                                    1/2 kijiko cha chai

Mdalasini                              1/2 kijiko cha chai

Siki au ndimu                       3 Vijiko vya supu
 
 
 
 
 * Ukipenda muache na ngozi bila ya kumchuna au mtoe ngozi.
 
 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
 
 
1.  Changanya tangawizi na thomu, pilipili mbichi pamoja na vitu vyote vingine katika kibakuli.

2.  Mpasue kuku kidogo (slit) kila mahali kuweka njia ya kuweka huo mchanganyiko wa rojo la kuvumbika.

3.  Mtie hilo rojo kila sehemu na muacha avumbike (marinade) kwa muda wa masaa mengi katika friji.

4.  Paka mafuta kidogo katika treya umuweke kuku, kisha mchome katika oveni moto wa 450º kwa muda wa dakika 45 hadi awive.

5.  Mtoe na umuweke katika sahani ya kupakulia ukipambia na saladi upendavyo.
 

No comments:

Post a Comment