Thursday, May 23, 2013

WANANDOA WA3 WALIOOANA SIKU 1 WASHEREKEA MIAKA 50 YA NDOA ZAO

Kusherehekea miaka 50 ya ndoa ni sherehe yenye furaha sana kwa kila waliofikisha miaka hiyo, zaidi ni pale unaposherehekea na rafiki zako wanne,
 
 ambao nao wananyanyua glasi kusherehekea sherehe yao wakiwa wanafikisha miaka hiyo hiyo ya ndoa zao, ila zaidi ni pale ambapo hao unaosherehekea nao, kama bahati walifunga  ndoa siku moja na wewe ndani ya kanisa moja.

 Norman na Mary Dickinson na Harry na Jean Winstanley, kutoka Flookburgh, Cumbria,  Alan na Anne Akrigg, kutoka Cark, Cumbria, wote walioana kwene kanisa la St John's lililopo  Flookburgh siku moja miaka 50 iliyopita mwaka 1963.

Tuesday, May 21, 2013

DAYNA AVUTIWA NA AFANDE SELE


Mwanamuziki  toka  mkoani  Morogoro  anayefanya  poa  kwa  sasa  na  ngoma yake  iitwayo  Leo  mwanadada  Dayna  Nyange  a.k.a  Mkali  wao,  amefunguka  na kumpigia  saluti
mwanamuziki  mkongwe toka  hapa  Morogoro Afande  Sele.

 '' kwa  kweli  siku  zote,  nimekuwa  nikimkubali  sana  Afande  sele  kwa  tungo zake  zenye  ujumbe,  lakini  kwa  wimbo  huu wa  Dini tumeletewa,  nampigia  saluti" Alisema Dayna na kuongeza kuwa,

 "Afande  ni  bonge  la msanii  na  huwa naskiliza  nyimbo  zake kwani  najuwa
nikiskiliza  nyimbo  zake  kuna  madini  napata,  lakini  sasa kaka  mkubwa  kwa  hapa  alipofikia  na kufikilia  kwa  kina juu  ya  wimbo  huu,  anastahili  kuwa mfalme wa  Rhyme,  waliompa  tuzo  hawakukosea".

 
Dayna ni mama wa mtoto mmoja na amewahi kutamba na nyimbo zake tofauti tofauti ikiwemo fimbo
ya mapenzi na nivute kwako aliyofanya na Barnaba.
 

HIKI NDICHO KILICHOMPATA MADAM RITHA


Akizungumza na Ijumaa Wikienda baada ya kuwa kimya muda mrefu ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru kwa kutoka salama.

Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo aliipata katikati ya Jiji la Dar  na kusababisha kuvunjika kwa kifundo ‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya hospitali kumuwekea ‘hogo’.

“Namshukuru Mungu kwanza kwa kunitoa salama katika ile ajali japokuwa sijapona vizuri,” alisema Madam Rita.
Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza kuwa alipopata ajali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Mifupa ya Moi lakini hali ilipokuwa kuwa mbaya alihamia katika hospitali moja ya Kichina ambapo kwa sasa amepata nafuu" Alisema Madamu
.

JAY Z AKANUSHA TAARIFA YA UJAUZITO WA BEYONCE.

Msanii mkogwe wa muziki wa Hip Hop duniani Jay Z amekanusha taarifa za ujauzito wa mke wake Beyonce kama zilizoripotiwa na vyombo vingi vya habari duniani.

Akizungumzia uvumi huo mtangazaji wa kipindi cha Ebro Darden  kilichopo New York alisema yeye alipopata taarifa hiyo alimtumia email Jay Z ikiwa katika hali ya kumpongeza kwa kutarajia kupata mtoto wa pili lakini baada ya muda alijibiwa kua sio kwel na hata alipomfanyia mahojiano alisisitiza sio kweli ni uvumi wa vyombo vya habari.

"Nilimpongeza lakini  Jay z alinijibu; sio kweli ni uvumi tu" Alisema Darden.
Uvumi huo ulianza baada ya Beyonce kuahirisha shoo aliyotakiwa kuifanya huko Ubelgiji kwa madai ya uchovu na upungufu wa maji.

 

Monday, May 20, 2013

WEMA SEPETU APATA BONGE LA DILI AWAFUNIKA MASTAA WOTE BONGO.

Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amepata mchongo wenye pesa ndefu kutoka kampuni ya nywele ya Darling Hair Tanzania.

Kwa mujibu wa meneja wake, Martin Kadinda mkataba huo utamfanya Wema awe staa mwenye thamani kubwa zaidi Tanzania ingawa amesema si kawaida yao kutaja kiasi cha fedha.

Deal hiyo itamuonesha Wema akiwa kama msemaji na sura wa Darling Hair Tanzania.




RECHO AJA NA VANNESA IN DILEMME

       Mcheza filamu wa kike maarufu Rachel Haule anatarajia kutoa filamu yake inatakayoitwa Vannesa in Dilemme.

      Akizungumza na Blog hii Recho alisema filamu hiyo imetengeneza katika kampuni yake inayoitwa Rasa Films Company ambayo amewashirikisha wasanii wakongwe kama Haji Adamu( Baba Haji), Jennifer Kyaka na wengine.