Tuesday, May 21, 2013

JAY Z AKANUSHA TAARIFA YA UJAUZITO WA BEYONCE.

Msanii mkogwe wa muziki wa Hip Hop duniani Jay Z amekanusha taarifa za ujauzito wa mke wake Beyonce kama zilizoripotiwa na vyombo vingi vya habari duniani.

Akizungumzia uvumi huo mtangazaji wa kipindi cha Ebro Darden  kilichopo New York alisema yeye alipopata taarifa hiyo alimtumia email Jay Z ikiwa katika hali ya kumpongeza kwa kutarajia kupata mtoto wa pili lakini baada ya muda alijibiwa kua sio kwel na hata alipomfanyia mahojiano alisisitiza sio kweli ni uvumi wa vyombo vya habari.

"Nilimpongeza lakini  Jay z alinijibu; sio kweli ni uvumi tu" Alisema Darden.
Uvumi huo ulianza baada ya Beyonce kuahirisha shoo aliyotakiwa kuifanya huko Ubelgiji kwa madai ya uchovu na upungufu wa maji.

 

No comments:

Post a Comment