Tuesday, May 21, 2013

DAYNA AVUTIWA NA AFANDE SELE


Mwanamuziki  toka  mkoani  Morogoro  anayefanya  poa  kwa  sasa  na  ngoma yake  iitwayo  Leo  mwanadada  Dayna  Nyange  a.k.a  Mkali  wao,  amefunguka  na kumpigia  saluti
mwanamuziki  mkongwe toka  hapa  Morogoro Afande  Sele.

 '' kwa  kweli  siku  zote,  nimekuwa  nikimkubali  sana  Afande  sele  kwa  tungo zake  zenye  ujumbe,  lakini  kwa  wimbo  huu wa  Dini tumeletewa,  nampigia  saluti" Alisema Dayna na kuongeza kuwa,

 "Afande  ni  bonge  la msanii  na  huwa naskiliza  nyimbo  zake kwani  najuwa
nikiskiliza  nyimbo  zake  kuna  madini  napata,  lakini  sasa kaka  mkubwa  kwa  hapa  alipofikia  na kufikilia  kwa  kina juu  ya  wimbo  huu,  anastahili  kuwa mfalme wa  Rhyme,  waliompa  tuzo  hawakukosea".

 
Dayna ni mama wa mtoto mmoja na amewahi kutamba na nyimbo zake tofauti tofauti ikiwemo fimbo
ya mapenzi na nivute kwako aliyofanya na Barnaba.
 

No comments:

Post a Comment