Friday, September 6, 2013

SNURA:NINA BIFU NA PESA TU.

MSANII maarufu wa filamu na mwimbaji Snura Mushi afunguka kuwa hajawahi kuwa na bifu na Wema wala Shilole zaidi ya kuwa na bifu na utafutaji pesa.

Akizungumza kupitia kipiti cha mitikisiko ya pwani kinachorushwa kupitia radio ya Times FM hivi karibuni Snura alisema hajawahi kuingia kugombana na msanii yeyote kama inavyosemakana bali yeye anafikiria kutafuta pesa zaidi.

Snura alisema Wema ni rafiki yake na hawakuwahi kugombana zaidi ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari ambazo sio za kweli na kuonyesha akuwa kuna ugomvi kati yao.

Mimi sina bifu na msanii yeyote wala haijawahi kutokea kuingia katika malumbano ninachowaza ni kutafuta pesa kwahiyo mimi nina bifu na pesa"Alisema

Snura alisema kwasasa anafikiria kuanza kufanya nyimbo ya pamoja na msanii maarufu wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuph ili kuongeza ladha ya muziki wake. 

Msanii huyo ambaye anatamba na nyimbo yake ya nimevurugwa alisema kwasasa anafanya juhudi za kujitambulisha zaidi ndani ya nchi kabla hajaanza kujitangaza kimataifa.

 

No comments:

Post a Comment