Wednesday, January 30, 2013

SASHA NA MARIE OBAMA WAMEKUWA WADADA

  Nafikiri ni zile genes za baba mrefu na mama mrefu wanaonekana wamekuwa na kurefuka Malia sasa ana miaka 14 na mdogo wake Sasha miaka 12

 

Na picha hii ilikuwa mwaka 2009 wakati baba yao Barack Obama akiapishwa kuwa raisi wa Marekani kwa awamu yake ya kwanza

Tuesday, January 29, 2013

PICHA ZA LULU WAKAT WAKUPATA DHAMANA

HATIMAE LULU YUKO NJE KWA DHAMANA
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu
Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.

URMILLA AT WORLI FESTIVAL 2013



TIMBULO AGEUKIA FILAMU


Baada ya kutesa kwenye anga ya muziki, msanii mahiri wa muziki wa Bongofleva nchini, Ally Timbulo, ameanza safari mpya kwenye tasnia ya filamu, huku wadadisi wa mambo wakisema msanii huyo anafuata nyayo za msanii wa kike Jack ambaye alikuwa mpenzi wake siku za nyuma.

Timbulo ambaye hivi sasa anatesa na wimbo wake wa Bado Kijana, tayari ameanza kazi ya upigaji picha wa filamu kali nay a kusisimua iitwayo World of Benefit

                Timbulo akiwa na Rose Ndauka kitandani katika Filam word of benefit
 


Ndani ya filamu hiyo msanii huyo anapambana na wakongwe wa tasnia hiyo ya filamu kama Mohamed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mama Mjata, Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka na Awadhi Saleh ambaye anakuja juu katika tasnia ya filamu kwa sasa.

“Nimepata bahati kufanya kazi na wasanii wakongwe, lakini pia nimepata bahati ya kusimamiwa na maproducer mahiri kama Selles Mapunda na Seleman Mkangara, hivyo naamini itakuwa kazi bora” alisema Timbulo.

Filamu ya World of Benefit imetayarishwa na mtayarishaji wa filamu Hamees Suba ‘Kemikali’ na inaongozwa na Selles Mapunda ‘Director of Directors’, akisaidiwa na Suleiman Mkangara ‘Striker’ kwa upande wa upigaji picha wapo wataalamu kutoka Bollywood chini ya kampuni ya Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam.



 





WASANII WAKIKE TANZANIA IGENI HAPA.

 Mwanadada kutoka Uganda anayejulikana kwa jina la Zari ni mzuri,tajiri,mfanyabiashara,mwanamuziki anasifika kwa kuendesha gari zenye gharama kubwa zaidi kuliko msanii yeyote kutoka Uganda.
  Pamoja na kuwa na biashara zingine nyingi Zari ni Mwenyekiti Mtendaji(CEO) wa brooklycitycollege.co.za(Chuo cha fani mbalimbali kilichopo Afrika Kusini.
 





/>

TAZAMA PICHA YA MJENGO WA MSANII JAGUAR NA MAGARI ALIYONAYO SASA


Monday, January 28, 2013

KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST WANUNUA NYUMBA KATIKA MAANDILIZI YA MTOTO


   Wakitarajia mtoto wao wa kwanza, Kim Kardashian na kanye west wameamua kuongeza nafasi ya eneo la kuishi
Mastaa hao ambao wanatarajia kupata mtoto mwezi Julai mwaka huu, wamenunua Italian style villa, ya 9,000 square-foot maeneo ya Bel Air, Los Angeles, kitongoji cha matajiri ilipokua inarekodiwa show ya Fresh Prince of Bel Air!


   Pamoja na mjengo huo kuwa na gym, movie theatre, saluni ya warembo kujiremba, bowling alley, kiwanja cha basketball, swimming pool mbili(ndani na nje ya nyumba,) mastaa hao wamepanga kubomoa ndani ya nyumba hiyo na kuidizaini upya iwe 14,000-square-food “dream home.”

  Nyumba hiyo mwanzoni ilikua kwenye list ikiuzwa kwa bei ya milioni $11.4 (TShs bilioni 18.4,) lakini ilipunguzwa bei mpaka dollar milioni 10.75 (TShs bilioni 17.3)
    Zifuatazo ni picha zinazoonyesha baadhi ya sehem katika nyumba hiyo.




LULU ATOKA LEO KWA DHAMANA

Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.

Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.

Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza
.

Sunday, January 27, 2013

TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUTATUA MIGOGORO

     Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Hemed Mgaza (katikati) Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge na Makanu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb). Kulia ni Mhe. Sadifa Juma Khamis, (Mb).Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa Wabunge watano kuhudhuria Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Jukwaa la Kibunge la nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Spika Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano huo.

 
Ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa PF –ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
         Picha ya pamoja ya maspika, Sekretarieti pamoja washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR.Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu (FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika.

Pongezii hizo zimetolewa leo na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo kwenye mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoa na watanzania kama wapenda amani barani Afrika

Hii ni kutokana na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC/Rwanda na kundi la M23, migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa Sudani na Sudani  Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini nay imepongezwa
. Bunge la Tanzania limewakilishwa na Spika wa Bunge ambaye ameongoza ujumbe wa wabunge watano ambao ni Mhe. Mussa Azzan Zunge, Mhe. Pauline Gekul, na Mhe Sadifa Juma. Wengine ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prude.