Tuesday, January 29, 2013

TIMBULO AGEUKIA FILAMU


Baada ya kutesa kwenye anga ya muziki, msanii mahiri wa muziki wa Bongofleva nchini, Ally Timbulo, ameanza safari mpya kwenye tasnia ya filamu, huku wadadisi wa mambo wakisema msanii huyo anafuata nyayo za msanii wa kike Jack ambaye alikuwa mpenzi wake siku za nyuma.

Timbulo ambaye hivi sasa anatesa na wimbo wake wa Bado Kijana, tayari ameanza kazi ya upigaji picha wa filamu kali nay a kusisimua iitwayo World of Benefit

                Timbulo akiwa na Rose Ndauka kitandani katika Filam word of benefit
 


Ndani ya filamu hiyo msanii huyo anapambana na wakongwe wa tasnia hiyo ya filamu kama Mohamed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mama Mjata, Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka na Awadhi Saleh ambaye anakuja juu katika tasnia ya filamu kwa sasa.

“Nimepata bahati kufanya kazi na wasanii wakongwe, lakini pia nimepata bahati ya kusimamiwa na maproducer mahiri kama Selles Mapunda na Seleman Mkangara, hivyo naamini itakuwa kazi bora” alisema Timbulo.

Filamu ya World of Benefit imetayarishwa na mtayarishaji wa filamu Hamees Suba ‘Kemikali’ na inaongozwa na Selles Mapunda ‘Director of Directors’, akisaidiwa na Suleiman Mkangara ‘Striker’ kwa upande wa upigaji picha wapo wataalamu kutoka Bollywood chini ya kampuni ya Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam.



 





No comments:

Post a Comment