A
Lakini inawezekana unajiuliza kwanini basi tumswalie Mtume صلى الله عليه وآله وسلم? Jibu la swali hakika ni refusana itaweza kuwa ni makala ndefu au kitabu kizima cha mas-alah haya. Lakini tutafupisha.
1. Kumtukuza Mtume wa mwisho;Lakini inawezekana unajiuliza kwanini basi tumswalie Mtume صلى الله عليه وآله وسلم? Jibu la swali hakika ni refu
Kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
ni katika kumtukuza kwani yeye ndiye Mtume wa mwisho, na hii ni neema
kwetu Ummah wa Kiislamu kujaaliwa sisi kuwa yeye ndiye Mtume wetu. Na
Allaah سبحانه وتعالى
Ametuambia kuwa sisi ni Ummah bora kabisa. Bila ya yeye tusingeliweza
kupata uongofu kamili (Qur-aan) na mafunzo ya Sunnah ambayo yametutoa
kizani na kutuingiza katika nuru.
Na ikiwa Allaah سبحانه وتعالى Mwenyewe Amemtukuza kwa kumtofautisha na Mitume mingine yote, kwani wote Amewaita kwa majina
2. Ni ibada kwetu;
Kwa
vile ni amri kutoka kwa Mola wetu kama tulivyoona katika aya hiyo ya
juu, na ndio maana tunamswalia mpaka kwenye Swalah zetu za fardhi na za
Sunnah, bila ya kumswalia Swalah haikamiliki.
عنْ
عبد اللَّه بن عمرو بن العاص ، رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول
اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ : (( من صلَّى عليَّ صلاَةً ،
صلَّى اللَّه علَيّهِ بِهَا عشْراً)) رواهُ مسلم
Imetoka kwa 'Abdullaah ibn 'Amru ibn Al-'Aasw رضي اللَّه عنْهُمَا kwamba kamsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم anasema, ((Atakayeniswalia Swalah moja Allaah Atamswalia (Atampa rahma Zake) mara kumi)) [Muslim]Maana ya Swalah ya Allaah سبحانه وتعالى na Malaika Wake
Swalah ya Allaah سبحانه وتعالى kwa waja Wake ni: Rahma na kuwasifu kwa Malaika.
Swalah ya Malaika kwa Waumini ni:
Du'aa na kuwaombea maghfirah.
Kupata daraja ya Pepo karibu naye Mtume صلى الله عليه وآله وسلم:
عن
ابن مسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ
وسَلَّم قال : (( أَوْلى النَّاسِ بي يوْمَ الْقِيامةِ أَكْثَرُهُم عَليَّ
صلاةً)) رواه الترمذي وقال : حديثٌ حسنٌ
Imetoka kwa ibn Mas'uud رضي اللَّه عنْهُ kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((watu wa mwanzo kwangu (watakaokuwa karibu yangu) siku ya Qiyaamah ni wale wanaoniswalia sana )). [At-Tirmidhy na kasema ni Hadiythi Hasan]
Vile
vile kumuombea Du'aa, mfano du'aa baada ya adhaan ni fadhila kwetu kuwa
atakayefanya hivyo atakuwa miongoni mwa atakayeombewa Shafa’ah na Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم siku ya Qiyaamah.
4. Kudhihirisha mapenzi yetu kwake ;
Muumini ni yule mwenye kumpenda khaswa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kabla ya kupenda chochote hata nafsi yake kwani ilipoteremka Aayah hii:
((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ))
((Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao)) [Al-Ahzaab: 6]
'Umar رضي الله عنه alisema kuwa yeye anampenda Mtume kuliko chochote ila nafsi yake. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
akamuambia 'Umar kuwa hadi ampende hata kuliko nafsi yake ndipo
yatakapothibitika mapenzi yake, naye 'Umar akakubali kuwa anampenda
kuliko hata nafsi yake. Kwa hiyo na sisi Waumini tuwe na mapenzi makubwa
ya kumpenda na dalili mojawapo ni kupenda kumswalia na kufuata
aliyokuja nayo na kujiepusha na aliyotukataza nayo ya uzushi (bid’ah) na
mengine.
((وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ))
((Na kwa hakika wewe una malipo yasiyokatika)) [Al-Qalam: 3]
Mbali
ya kuwa ni malipo yake kwa sababu ya Utume wake na kufikisha ujumbe kwa
tabu na mashaka, vile vile kumswalia kwetu kila siku