Tuesday, August 27, 2013

RAY C AINGIA GYM.

Zaidi ya sauti yake na uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo zinazoshikika kiurahisi, umaarufu wake mwingine mkubwa toka enzi hizo ni kiuno bila mfupa kwa jinsi alivyokua akicheza nacho….. ni uwezo uliofanya mpaka maneno ya kiuno bila mfupa yakapata umaarufu kupitia yeye.

Siku kadhaa tu baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki kama zamani, Ray C akiwa ametoka kwenye matibabu ya matumizi ya dawa za kulevya… ameanza kujipanga kupunguza unene alionao ili awe mwepesi zaidi ya alivyo sasa ili kila kitu kiende kama kilivyokua.

Ray C akipiga story na fans wake alisema “Mauno ni nyonga si manyama”, hii ni moja ya sababu za msingi sana zilizomfanya Rehema Chalamila kuingia gym kuanza mazoezi.






Monday, August 26, 2013

BAD LUCK IKO NJIANI


Ile Sinema iliomshirikisha miss Tanzania mwaka jana Salha Israel, Muda si mrefu itaingia mtaani kwa kishindo inayokwenda kwa jina la BAD LUCK Wadau mzigo huu si wa kuukosa kama kawaida ya RJ Company uwa hawabahatishi kwenye kazi.

JINSI YA KUANDAA KATLES ZA SAMAKI


 

Viazi    5 kiasi

Tuna    2 vikopo

Karrot 1

Pilipili             Nusu

Thomu          ½ kijiko cha chai

Pilipili          kiasi

Chumvi        kiasi

Ndimu         kiasi

Unga wa ngano     ½ kikombe

Yai              1

Mafuta ya kupikia        Kiasi      

                                                               

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Menya Viazi uvichemshe na chumvi.

2.      Vikiwiva vichuje maji, viponde ponde, vilainikie – weka kando

3.      Chuna karrot ziwe kama chicha, kata pilipili mboga  nyembamba nyembamba,   fungua vibati vya Tuna kamua majia yake mwaga. 

4.      Changanya Tuna, karrot, pilipili mboga, thomu, pilipili kali, chumvi, ndimu, kisha uchanganye na viazi ulivyoviponda. Hakikisha vimechanganyika vizuri.

5.      Tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo unalopenda kama la yai au duwara ukimaliza weka pembeni.

6.      Changanya unga na maji uwe mzito mzito tena uchanganye vizuri na yai.

7.      Weka karai katika moto, mimina mafuta kama ya maandazi, kisha chukua vidonge chovya katika unga uliochanganywa yai  na utumbukize ndani ya mafuta yaliopashika moto vizuri.

8.      Ziwache mpaka zibadilike rangu, uzitoe. Tayari kwa kula. 

YANAYOJIRI KATIKA FIESTA MIKOANI.

Wasanii mbalimbali wakiwa katika safari zao za Serengeti Fiesta 2013.
                     Msanii Diamond Platinum na Lina wakiwa katika pozi
                     Mmoja wa memba wa makomandoo akiwa na Lina
                                                      Recho katika pozi
                                   Shilole katika pozi na wasanii wengine