Viazi 5 kiasi
Tuna 2 vikopo
Karrot 1
Pilipili Nusu
Thomu ½ kijiko cha chai
Pilipili kiasi
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Unga wa ngano ½ kikombe
Yai 1
Mafuta ya kupikia Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Menya Viazi uvichemshe na chumvi.
2. Vikiwiva vichuje maji, viponde ponde, vilainikie – weka kando
3. Chuna karrot ziwe kama chicha, kata pilipili mboga nyembamba nyembamba, fungua vibati vya Tuna kamua majia yake mwaga.
4. Changanya
Tuna, karrot, pilipili mboga, thomu, pilipili kali, chumvi, ndimu,
kisha uchanganye na viazi ulivyoviponda. Hakikisha vimechanganyika
vizuri.
5. Tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo unalopenda kama la yai au duwara ukimaliza weka pembeni.
6. Changanya unga na maji uwe mzito mzito tena uchanganye vizuri na yai.
7. Weka karai katika moto, mimina mafuta kama
ya maandazi, kisha chukua vidonge chovya katika unga uliochanganywa yai
na utumbukize ndani ya mafuta yaliopashika moto vizuri.
8. Ziwache mpaka zibadilike rangu, uzitoe. Tayari kwa kula.
No comments:
Post a Comment