Vipimo:
*Kuku mzima 1
Tangawizi na thomu 1 kijiko cha supu
Mtindi 3 vijiko vya supu
Rojo la ukwaju 2 Vijiko vya supu
Pilipili mbichi 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Bizari ya jiyrah (cummin poda) 1 kijiko cha chai
Bizari ya dania (coriander poda.1 kijiko cha chai
Paprika 1 kijiko cha chai
Kungu manga ya unga 1/2 kijiko cha chai
Hiliki 1/2 kijiko cha chai
Mdalasini 1/2 kijiko cha chai
Siki au ndimu 3 Vijiko vya supu
* Ukipenda muache na ngozi bila ya kumchuna au mtoe ngozi.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
2. Mpasue kuku kidogo (slit) kila mahali kuweka njia ya kuweka huo mchanganyiko wa rojo la kuvumbika.
3. Mtie hilo rojo kila sehemu na muacha avumbike (marinade) kwa muda wa masaa mengi katika friji.
4. Paka mafuta kidogo katika treya umuweke kuku, kisha mchome katika oveni moto wa 450ยบ kwa muda wa dakika 45 hadi awive.
5. Mtoe na umuweke katika sahani ya kupakulia ukipambia na saladi upendavyo.