Friday, February 15, 2013

ALICHOKISEMA PREZO BAADA YA TAARIFA YA KIFO CHA MPENZI WAKE GOLDIE.

 


Baada ya taarifa za msiba kusambaa kila sehemu Africa na dunia kuhusu kifo cha mwanamuziki Goldie Harvey, hatimaye aliyekuwa mume mtarajiwa wa marehemu Goldie, Prezzo ameonyesha kuguswa kwake na kifo hicho cha mpenzi wake.

Prezzo ameandika maneno katika ukurasa wake wa facebook yakionesha ni jinsi gani ameguswa na msiba huo. Hapa chini ndio maneno aliyoandika msanii huyo...



_______________________________

Thursday, February 14, 2013

BREAKING NEWS;GOLDIE WA PREZZO NA BIG BROTHER AFARIKI DUNIA


Prezzo na Goldie
PREZZO AKIWA NA MPENZI WAKE GOLDIE ( ENZI ZA UHAI WAKE)
Ni taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page zake za facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana.

Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria, hali yake ya afya ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe hospitali ambako hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.

Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.

Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.

Wednesday, February 13, 2013

HUYU NDIYE MSANII WA TMK ALIYEAGA DUNIA


Msanii kutoka kundi la TMK WANAUME FAMILY anatejulikana kama BK leo hii amefariki dunia kwenye hospital ya MUHIMBILI.

Imeelezwa kuwa BK kabla yakukutwa na mauti alikua akisumbuliwa na homa ya matumbo na kupelekwa hospital ya TEMEKE.Hali ilizidi kua mbaya alihamishwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo vipimo vilionyweshwa kuwa alikua na tatizo la kuvimba ini ugonjwa uliopelekea kifo chake.

Uongozi kesheridhiwani.blogspot.com unatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki .

WOLPER AELEZEA MAISHA YAKE NJE YA FILAMU


   MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolper anaamini mafanikio hutokana na juhudi, kujituma pamoja na kutimiza malengo yako uliyojiwekea kwa kipindi ulichokusudia

Msanii huyo wa filamu alielezea maisha yake yako nje ya Tasnia ya filamu.

Wolper mbali na kuigiza pia yeye ni mcheza netiboli katika timu ya bongo movi akiwa anachukua nafasi ya mfungaji 'GS' huku akiwa tishio kwa timu pinzania kwa uwezo alionao na jinsi anavyoweza kutumia urefu aliokuwa nao kwa kufunga magoli mengi

Alianza kucheza netball  akiwa shuleni na huko ndipo alipopata ujuzi wa mchezo huo ambapo mpaka sasa ameweza kuwa tishio kwa kuumudu mchezo huo na kuweza kuisababishia ushindi kwa timu anayoichezea

Alisema kuwa anapata muda wa kutosha kufanya mazoezi kila siku jioni na asubuhi hivyo mazoezi yanamsaidia kujenga mwili wake pia na kumpa pumzi zinazomsaidia kucheza kipindi chote bila ya kupumzika mpaka mwisho wa mchezo

Aliendelea kusema kuwa kwa upande wake anathamini sana mazoezi kwani yanamfanya kuzidi kuwa imara na pia hutumia mazoezi kwake ni kama dawa ya kuondoa uchovu katika mwili wake

Wolpa aliweka wazi kuwa kama ingekuwa si muigizaji basi angekuwa mchezaji mzuri wa netball na angeongeza nguvu katika hilo na kuweza kuchezea timu kubwa na anaamini kuwa angefanya vizuri kwenye upande huo

 Hatoweza kusahau siku alipoumia vidole vya mikono kwenye mechi iliyokuwa inachezwa katika viwanja vya Leaders Club na aliweza kuendelea kucheza mchezo huo na hatimaye waliibuka washindi katika mechi ya kujipima

Mbali na kucheza netball  pia msanii huyo ni bingwa wa kuogelea, huku akidai kuwa muda wake mwingi wa mapumziko anautumia kuogelea ili kuweka mwili wake imara

 Mara nyingi huwa anaratiba ya nini afanye muda gani na kipi kifanyike wakati gani hiyo ndiyo moja ya kitu anachoamini kuwa kinampa mafanikio makubwa katika maisha yake

Wolper huwa hapendi kuwa na makundi ya watu hivyo hawezi kuamua kwenda kukaa bar kama hana kazi ya kufanya kwa sababu ratiba yake inakuwa imejaa muda wote ule

Wolpera ambaye pia alikuwa anafanya biashara ingawa sasa anajipanga kuianzisha tena biashara yake ili maisha yake yaendelee kuwa yenye mafanikio kwa juhudu anazozifanya

 pia, anapenda kusoma vitabu muda wa mapumziko zaidi kuliko kwenda kukaa bar na marafiki ambao kwake anahisi labda hawana mafanikio ingawa si kila rafiki ni mwema au ni mbaya hivyo kwa upeo wa kiubinadamu huwezi kutambua hilo kwa haraka


 
Wolper ni msanii wa filamu ambapo alianza kuigiza mwaka 2009 na filamu iliyomtambulisha ni AMAZANGU AMAZAO kwa sasa anatamba na filamu nyingi ikiwemo ya NDOA YANGU aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba.

YOUNG D AFUNGUKA KUHUSU TATOO ZAKE




Rapper Mkali wa Bongo ambae kwasasa anaetikisa na ujio wake mpya ambao amemshirikisha Mr.Blue ngoma inayojulikana kama "Hujali" ambayo uzinduzi wake ulifanyika J.pili ya terehe 10 pande za kigamboni hapa tunamzungumzia.
      Young Dee a.k.a Young DSM amefunguka katika mahojiano kua Hajutii kujichora Tattoo Shingoni na mkononi kwa kudai kua yeye sio mtoto tena sasa hivi umri wake unaruhusu kufanya chochote nafsi yake inavyomwambia na sababu kubwa ni kua Tattoo hizo zote zina maana kubwa katika mwili wake akielezea
    Alisema "Kiufupi nizungumzie tattoo yangu hii ya mwisho ambayo ndo naipenda sana kulingana na maana yake, ipo mkono wa kulia ni mkono ambao ninaoutumia mara zote na nimeandika OMG ambapo chini ya kila izo herufi tatu kuna maneno yake yanii O-ver everything My hand is G-ot to make it easy....


Tuesday, February 12, 2013

AMBER ROSE KUTARAJIA MTOTO MUDA WOWOTE

Star wa muziki wa Hip Hop duniani Wiz Khalifa akiwa anaonekana mwenye furaha kila anapokua na mama wa mtoto wake mtarajiwa Miss Amber Rose wawili hao wakiwa wanatarajia kupata mtoto muda wowote kwanzia sasa lakini hawakuweza kukosa Tunzo za Grammyz ambapo Amber akionesha Support kwa mpezi wake ambae alikua nominated kwenye tunzo Hizo…

DAILY NATION LA KENYA LAWATAJA WASANII WATANO WA BONGO FLAVA MATAJIRI ZAIDI

Gazeti maarufu la nchini kenya Daily Nation limetoa orodha ya wasanii watano wa bongo flava matajiri zaid.hivi ndivyo lilivyofanya uchambuzi huo.
NASSIBU ABDUL(DIAMOND)
   He stayed in shadow for long looking for break but now that the limelight has been trained on him,he has proved that belongs at the top of the music chats.He finally made a debut in 2009 with his hit song "kamwambie".He is one of the most expensive musicians not just in Tanzania but the region and his does not seem to put promoters off as he 0n the stage on weekly basis.Wants him for a show,you will have to pay him $4000 (sh 350,000) and that's after a bargain.
   This has enable him make a fortune for himself in a very shot period of time.he owns masions in Tanzania,acres of land,car and shop.
JOSEPH HAULE(PROFESSOR JAY)
  He began his music career in 1990 with a group called the Hard Blasters.It's this band that started the music style know as"MUZIKI WA KIZAZI KIPYA".the artist has acqured his wealth throgh the many he does internationally.
  He owns beachfront mansion which has an in builts studio,drive a modest Toyota spacio but dont let that fool you,its not that can't afford fuel because he makes good money from his music and owns several parcel of land is also a serious investor.
JUDITH WAMBURA(LADY JAY DEE)
    She started her music career at the of the 1999 she is one of most respected Tanzania artst and has remained humbled through her success.she is very hard working and his led her to accumulate a good fortune to her name
     Her garage pays homage to Nissan Murano,a Toyota coaster minibus,Toyota prado among others.she of course cant own all those and rest.she own a mansion she also invests hearily and own a band by the name Machozi.
AMBWENE YESAYA(AY)
   He started his music back in 2000 with the group East coast.The group later split and he continued to do his also solo music together with his close friend Hamisi Mwijuma(mwana FA).they are still close friend and have been friend for more than ten years.
  He is owner of Unity Entertaiment company which produces programmes like the famous "mkasi"which is broadcasted on East Africa Television.He recently did a collabo with Lil Romeo that got some good reception across the continent.

    JUMA NATURE
   He is one of long time who are still relevant in music scene.He has been able to make a name for him self since his day in the male group TMK when he was under Mkubwa Fela.He later and formed his own group called 'WANAUME HALISI".
  He own a fleets of taxis that operate in Dar es salaam he own acres of land and home

RADI YA PIGA KANISA LA ST PETER'S BASILICA SAA KADHAA BAADA YA PAPA BENEDICT KUTANGAZA KUJIUZULU.

Je? hii ni ishara kutoka kwa mungu? kwa sababu amini usiamini saa kadhaa baada ya papa Benedict xvi kutangaza kujiuzulu radi kubwa ilipiga kwenye kanisa la st peter Basilica.
Papa benedict aliwastua mabilion ya waumini wa kanisa katoliki dunian kwa kutangaza kuwa ajiuzulu mwishoni mwa mwezi huu papa huyo mwenye umri wa miaka 85 amekua kiongozi wa kanisa hilo tangu mwaka 2005.

HAWA NDIO WASANII WALIOTANGAZA KUJITOA PAH1

 

    Aika Aka First Lady wa Pah 1 ametangaza Rasmi Kujitoa kwenye kundi la Pah 1 pamoja na Rapper na Producer wa Pah One `Nah Real'. Aika amesema kutokuelewana kwenye kundi ndio kumefanya ajitoe na hajawahi kuongelea jambo hili mapema kwani hakutaka watu wahukumu upenda wowote wa kundi hilo nakuonekana ndio lenye makosa. Pia Aika amesema Nah Real pia ni solo Artist na yeye na Nah Real Hawaja vunja Kundi Hilo na wamechukizwa na taarifa kuwa mapenzi yake na Nah Real Ndio yamevunja kundi hilo. Wimbo wa kwanza wa Nah Real Na Aika utatoka tarehe 14 Mwazi Huu.

Monday, February 11, 2013

PHOTOS OF KENYA'S TONIGHT PRESIDENTIAL DEBATE STAGE

Photos of the stage on which Kenya’s presidential debate will take place tonight. It looks absolutely beautiful. Let’s hope the candidates will bring something significant to the table and be as impressive in challenging each other and in informing the masses.

People standing behind the pulpit during presidential debate rehearsal


PAPA BENEDICT XVI KUJIUZULU

 


Papa Benedict XVI
 Habari kutoka Vatican leo hii zimethibitisha kuwa Papa Benedict XVI atajiuzulu kutoka katika nafasi yake hiyo Februari 28 mwaka huu kutokana na Umri wake kuwa mkubwa mno na kupelekea kupungua uwezo wa utendaji wa kazi zake.
Father Federico Lombardi ambaye ndiye msemaji wa Papa ametoa taarifa hizi rasmi leo  kwa vyombo vya habari, ikiwa ni ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Papa kwa makadinali wa kanisa hilo duniani.

Papa huyu atatimiza umri wa miaka 86 tarehe 16 mwezi April na alichaguliwa kushika nafasi hii mwaka 2005 akiwa mjerumani wa 6 kushika nafasi hiyo ya juu katika kanisa Katoliki na wa kwanza kabisa kuhudumia kanisa kama papa kutokea karne ya 21

CHRIS BROWN APATA AJALI

  Wikiendi hii iliyopita msanii Chris Brown alikuwa katika hali sio nzuri ambapo alipata ajali na gari yake ya aina ya PORSCHE .Tukio hilo lilitokea alivyokuwa anawakwepa PAPARAZZI na kukimbilia kwenye gari lake ndipo alipoanza kuondoka ndo akagonga gari ambalo lilikuwa mbele yake.

                                      




Sunday, February 10, 2013

OFFICIAL RELEASE(Feza Kessy)-Amani ya Moyo

 
)
     Baada ya kutambulishwa rasmi na Label ya Unity Entertaiment ambayo inasimamiwa na msanii Ay,track ambayo ilikuwa inasubiriwa kutokakwa mwanadada aliyewahi kufanya vizuri kwenye mitindo Feza Kessy sasa kutoka Jumatatu 11.2.2013
    Track hiyo itakwenda kwa jina la Amani ya Moyo  ambayo imefanyika katika Studio  za Mpo Africa chini ya producer Ben Mwamba na kufanyiwa mixing na Marco Chali...Kaa tayari kwa ujio wake.