Monday, June 24, 2013

RIYAMA ATOA SIRI YA KUPEWA TUZO NA KAMPUNI YA STEPS INTERTAIMENT

Msanii maarufu wa filamu Riyama Ally 'Riyama' aeleza siri ya kufanya vizuri katika tasnia ya uigizaji na kudumu kwa muda mrefu.
Alipozungumza na SAYARI YA WANAWAKE hivi karibu Riyama alisema kuwa ni juhudi zake binafsi katika uigizaji pamoja na kuheshimu sana kazi yake.

Riyama alisema zipo sababu nyingi lakini yeye binafsi anaipenda sana kazi yake ya uigizaji na akaamua kuwekeza juhudi zaidi ili kuweza kuwaburudisha na kwaelimisha wapenzi wake pindi watakaponunua kazi zake.
"Naipenda kazi yangu ya uigizaji,najiheshimu na nawaheshimu niniaofanya nao kazi pamoja na kuwa na nidhamu ndio vinanifanya nionekana tofauti"Alisema
Mbali na kufanya vizuri katika kazi zake mbalimbali pia amejipatia tuzo ya msanii bora wa kike msaidizi zilizotolewa hivi karibuni kupitia  kampuni ya step intertaiment.
Mwigizaji huyo ambaye hana skendo aliongeza kuwa amefurahi kupata tuzo hiyo na amemuongezea ari ya kuzidi kufanya vizuri katika kazi zake atakazozitoa.
Riyama aliwahi kufanya vizuri katika kazi mbalimbali ikiwemo ya fungu la kukosa na sasa anatamba na Filamu ya The dream aliyoshirikiana na wasanii wengine akiwemo mwimbaji Khadija Kopa.

 

No comments:

Post a Comment