Wednesday, March 6, 2013

SABABU ZA KUJERUHIWA KWA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ZATAJWA

                          (waziri wa afya na ustawi wa jamii Hussein Mwinyi akimjulia hali)
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bwana Theophil Makunga amesema maelezo ya awali yanaonyesha kuvamiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa hilo kunatokana na sababu za kazi yake ya uandishi wa habari.
      Makunga amesema Bwana Absalom Kibanda amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana na kumjeruhi baadhi ya sehemu ya mwili wake wakati akirejea nyumbani.
      Tukio hili lililotokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya nyumbani kwake mbezi beach jijini Dar Es Salaam linahusishwa na sababu za kitaaluma kama anavifafanua bwana Theofil Makunga…
      Hussein Bashe ni mkurugenzi Mtendaji wa News Habari Corporation ofisi mwajiri wa Kibanda anasema hakuna kifaa cha kazi kilichoibiwa katika tukio hilo na kuwa wanafanya taratibu kumsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
     Miongoni mwa viongozi waliofika kumtembelea ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Hussein Mwinyi amesema serikali imesikitishwa na kitendo hicho.
    Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar Es Salaam Sulemani Kova amesema wanashirikiana na makao makuu ya polisi katika kufanya upelelezi wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment