HALI ya sintofahamu imewakumba wahitimu wa kidato cha sita nchini, na kuibua malalamiko miongoni mwa wahitmu hao, kufuatia taarifa iliyochapishwa na mtandao wa Jeshi la Kujenga Taifa 'JKT', ikiwataka wahitimu hao kwa ajili ya awamu ya tatu ya mafunzo maalumu, ikiwa ni mwendelezo wa program maalum ya kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wanafunzi wote wanaohitimu kidato cha sita nchini, kabla ya kujiunga na masomo yao ya elimu ya juu.
Taarifa hiyo, ilitanabaisha kuwa ni wito kwa ajili ya awamu ya tatu ya mafunzo hayo, ambapo wametakiwa kuwasili katika kambi walizopangiwa mnamo tarehe 28 septemba mwaka huu, ikiwa imetanguliwa na awamu ya kwanza na ya pili, zilizofanyika mapema mwezi March na June mwaka huu.
Punde tu baada ya kuwekwa kwa agizo hilo, Wahitimu wengi walionyesha kushangazwa na taarifa hiyo, ambapo walihoji ni utaratibu gani unaotumika wa kushtukiza ilihali tayari tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imeshatoa chaguzi za wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali na wapo ambao wamesharipoti kwenye vyuo hivyo.
Huku wakionesha wazi kuchanganywa na taarifa hiyo, baadhi ya wahitimu wameelezea kukerwa kwao na uchachafishaji huu uliofanywa na vyombo hivi vikubwa nchini, na kuhoji ni upi ushirikiano baina ya Tume ya vyuo Vikuu na Jeshi la Kujenga Taifa kituendaji.
Hata hivyo, wapo pia waliodai kuwa pengine taarifa hiyo ilichapishwa bila kukusudiwa kutokana na makosa ya kiufundi (technical errors), Hivyo kuwataka wahusika kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo haraka, Jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika hivyo hali ya sintofahamu kuendelea kutamalaki!
Mtandao huu ulifanikiwa kutembelea mtandao huo (www.jkt.go.tz), na kushuhudia taarifa hiyo ambayo imedaiwa kuchanganya vichwa vya wanafunzi hao, Huku wengi wao wakijiuliza, waende wapi, Kambini au Vyuoni?????
No comments:
Post a Comment