Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

Friday, June 21, 2013

HOUSEGIRL ANUSURIKA KUJIRUSHA KWENYE GHOROFA KWA KUOGOPA MOTO

 HAUSIGELI ambaye jina lake halikupatikana mara moja, nusura ajirushe chini kutoka ghorofa ya pili kwa kile kilichodaiwa kuwa aliogopa moto mkubwa uliozuka katika jengo la jirani na ghorofa alilokuwemo.

 Tukio hilo lilijiri mapema asubuhi ya Juni 18, mwaka huu kwenye makutano ya Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa majirani, baada ya kuona moto huo ulioambatana na wingu zito la moshi ukitoka kwenye jengo la jirani, hausigeli huyo alitoka dirishani na kutaka kujirusha chini bila kujali nguo zilizokuwa zikimvuka katika purukushani hiyo.
Alifanikiwa kukaa kwenye sehemu ya ukingo wa ghorofa hilo na kujiandaa kwa tukio la kwenda chini akiamini atakuwa amejiokoa na moto huo.
Hata hivyo, bosi wa hausigeli huyo alipoona zoezi hilo la hatari alitoa mkono dirishani na kumvutia ndani mfanyakazi wake huyo tukio ambalo lilijiri muda mfupi kabla ya Kikosi cha Zima Moto kufika na kufanikiwa kuuzima bila kujeruhi mtu.

Monday, February 4, 2013

MWANSITI NA VITU ANAVYOMILIKI.

       Hitmaker wa nalivua pendo na mapito,MWANSITI ALMASI ameeleza mafanikio aliyoyapata kupitia kazi yake ya muziki ambapo amefanikiwa kununua gari lenye thamani ya milioni 16 na mjengo anaomalizia maeneo ya mbezi beach jijini Dar es salaam.
   Kupitia kipindi cha amplifaya cha clouds fm mwansiti alisema nyumba hiyo yenye vyumba 5 inatarajiwa kumalizika baada ya miezi michache ijayo.