Saturday, March 2, 2013

RADO AJA NA FALL IN LOVE

 

Simon Mwakipagata
Rado mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
FILAMU ya Fall in Love ya Simon Mwakipagata ‘Kaptorado’ inatarajia kumweka vizuri msanii huyo baada ya kubadilika katika staili yake ya uigizaji, Rado mara nyingi upendelea kuigiza filamu zinazomweka katika nafasi za kitemi lakini katika filamu ya Fall in love anaigiza kwa aina nyingine ya kimapenzi, Rado mwenyewe anasema kuwa amepanga kila anapotoa filamu amelenga kubadilika badilika kwa ajili ya kuhakikisha wapenzi wake wanapata filamu bora na za kuburudisha.



Rose Ndauka
Rose Ndauka pia yupo
Haji Salum

Mboto mchekeshaji mahiri naye yupo katika filamu Fall in Love.


 


  • Simon Mwakipagata

 
“Filamu yangu ya Fall in Love imekuja kivingine maana wapenzi wa filamu wamezoea kumuona Rado akiwa na misheshe mwanzo mwisho lakini humu ni mambo mazito ya kimaisha mahusiano na kila kitu, nilikuwa nimepanga mwaka uliopita nilifanya kazi kwa ajili ya watoto nikatoa filamu ya Maduhu nikishirikiana na watoto walioibuliwa na marehemu Kanumba, sasa nimerudi na watu wazima kielimu zaidi kupitia filamu ya Fall in Love,”amedai Rado.
Msanii huyo amejigamba kwa kusema kuwa kazi yake hiyo imeandaliwa kwa umakini zaidi jambo linalomfanya ajivunie filamu hiyo kwani amefanya kazi kubwa kuanzia uandishi wa muswada wake, huku pia akiwasifia waigizaji wake kuigiza katika kiwango cha juu, wasanii
walioshiriki katika filamu hiyo ni Rose Ndauka, Salum Haji aka Mboto mchekeshaji anayefanya vizuri katika filamu hasa sehemu za kuchekesha.



BOB JUNIOR ON HIS EVER FIRST EUROPEAN TOUR

 



GOING TO CITIES AS NAPOLI IN ITALY,HELSINKI,FINLAND,COPENHAGEN,DENMARK,HOLLAND AND FRANKFURT GERMANY,,ALL THE BEST!!

MILEY CYRUS(HANNA MONTANA) ABADILI STYLE YA NYWELE



STAR WA DISNEY CHANNEL..  MILEY CYRUS AU MAARUFU KWA JINA LA HANNA MONTANA AMEFUNGUKA KUWA HUU MUONEKANO WAKE MPYA WA NYWELE FUPI ATADUMU NAO KWA MUDA MREFU NA HANA MPANGO WA KUWEKA NYWELE NDEFU..
 ANASEMA MPENZI WAKE ANAZIPENDA NYWELE FUPI NA ANAONA HAZIMPI UZITO.... KAMA NDUGU YANGU U DONT LIKE IT NA WEWE NI FAN WAKE JITAHIDI KUZIPENDA MAANA HANA PLAN YA NYWELE NDEFU ANYTIME SOON.


Friday, March 1, 2013

FIFA YAWASILISHA MAREKEBISHO 10 YA KATIBA KWA WARAKA


Rais wa TFF, Leodegar Tenga
Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limetuma mapendekezo 10 ya marekebisho ya Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka.
Mapendekezo hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320, ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga kura ya ndiyo au hapa. 
Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Baadhi ya mapendekezo hayo ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). 
Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi wathibitishwe na FIFA Congress.
Muundo wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA). 
Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura.
Uchaguzi wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama wanachama kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi; kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe.
Uwakilishi wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi katika mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.

JINSI YAKUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI

 

Kama tunavyojua chunusi hazitakiwi kusababisha makovu lakini ukitumbuaji au kubadua chunusi kunasababisa makovu kwenye uso au mwili.Kama unamakovu ya chunusi kuna namna nyingi ya kuweza kuyaondoa makovu hayo lakini treatment zake zinaweza kuwa na maumivu sana au za ghali sana lakini kuna njia za kihalisia za kuweza kuondoa makovu hayo.1.Paka bleach cream kwenye sehemu zenye makovu ambapo cream hii husaidia kuyangarisha makovu2.Pia unaweza kutumia kuondoa ngozi ya juu (Exfoliate) kwa kutumia facial body scrub kwa sehemu zile zenye makovu lakini inategemea na sehemu gani ya mwili. Uondoaji huu wa layer ya juu (Exfoliate) unaweza kufanya angalau mara mbili kwa wiki.
3.Tumia product ambazo zina `hydroxy acids` hii acid hutokea kihalisia na hutibu ngozi yako na vile vile ngozi yako itaonekana younger and smoother, na makovu ya chunusi hupotea. Unaweza kupata hydroxy acids tofauti tofauti za skin care products kam vile cleansers, lotion na serums.4.Pia unaweza kumassage makovu ya chunusi kwa maana massage hushauriwa kwa ajili ya mzunguko wa damu ambapo husaidia hufika katika sehemu zile zenye makovu ambapo tunaambiwa massage pia husaidia sana kuvunja scar tissue.5.Vile vile kuna diet za kufanya ambazo husaidia kuondoa makovu kwenye ngozi ambapo unatakiwa kula vyakula vyenye vitamins na nutrition vinasaidia kutengeneza ngozi yako kuwa na afya.Kama lishe yako sio nzuri ngozi yako pia haitaweza kujitengeneza yenyewe (heal its self)na itakua ngumu kuondoa makovu kwenye mwili.6. Waweza pia kutumia cream maalumu kwa ajili y akuondoa makovu mwilini na crea hizi hupatikana sehuku nyingi na husaidia sana kuondoa makovu ya chunusi.Unachotakiwa ni kufuata maelekezo ya cream unayotumia ambapo utatakiwa kupata kwa muda kadhaa kwa muda wa wiki 12 kabla ya kuona matokeo.

Thursday, February 28, 2013

RIHANNA COVERS ELLE MAGAZINE UK APRIL 2013


 

MTARAJIWA WA ROSE NDAUKA AJICHORA TATTOO KUONYESHA MAPENZI YA DHATI

 





MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka afunguka juu ya tatoo  alizochora mchumba wake Mariki Bandawe, zinazoonyesha mchoro wa kopa . Alisema kupitia mchoro huo ni dhahiri kuwa mchumba wake amedhihirisha kuwa na mapenzi ya dhati


Rose alilazimika kufunguka juu ya hilo baada ya kupokea maswali mengi kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii 'Facebook' baada ya kuituma picha hiyo inayomuonyesha mchumba wake akiwa na mchoro kwenye bega lake la kushoto


Akizungumza na jarida la Maisha Rose alisema kuwa mchoro wa mchumba wake ni dhahiri kuwa ana mapenzi ya dhati kwani ni wanaume wachache wanaweza kufanya kitendo alichokifanya yeye na kutuma picha kama hiyo ambayo inaonekana na watu wengi


"Unajua mpaka mtu inafikia hatua ya kuweka wazi ni kwamba unajiamini na chaguo lako na pia kwa upande wangu inaonyesha kunijali na kunilinda na baadhi ya magonjwa maambukizi kwa kutojihusisha na mwanamke mwingine," alisem Rose


Pamoja na hayo alizungumzia juu ya harusi yake ambayo amesema kuwa muda ukifika ataweka wazi tarehe na mwezi wa siku yao ya kufunga ndoa


Picha hiyo ilionekana kuleta utata baada ya mchumba wake kuituma picha kwenye mitandao ya kijamii 'facebook' huku baadhi ya mashabiki wakituma maoni yao juu ya picha hiyo na kutaka kufahamu nini maana ya alama iliyokuwepo kwenye picha