Rado mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
FILAMU ya Fall in Love ya Simon Mwakipagata ‘Kaptorado’ inatarajia
kumweka vizuri msanii huyo baada ya kubadilika katika staili yake ya
uigizaji, Rado mara nyingi upendelea kuigiza filamu zinazomweka katika
nafasi za kitemi lakini katika filamu ya Fall in love anaigiza kwa aina
nyingine ya kimapenzi, Rado mwenyewe anasema kuwa amepanga kila anapotoa
filamu amelenga kubadilika badilika kwa ajili ya kuhakikisha wapenzi
wake wanapata filamu bora na za kuburudisha.
 |
Rose Ndauka pia yupo |

Mboto mchekeshaji mahiri naye yupo katika filamu Fall in Love.
“Filamu yangu ya Fall in Love imekuja kivingine maana wapenzi wa
filamu wamezoea kumuona Rado akiwa na misheshe mwanzo mwisho lakini humu
ni mambo mazito ya kimaisha mahusiano na kila kitu, nilikuwa nimepanga
mwaka uliopita nilifanya kazi kwa ajili ya watoto nikatoa filamu ya
Maduhu nikishirikiana na watoto walioibuliwa na marehemu Kanumba, sasa
nimerudi na watu wazima kielimu zaidi kupitia filamu ya Fall in
Love,”amedai Rado.
Msanii huyo amejigamba kwa kusema kuwa kazi yake hiyo imeandaliwa kwa
umakini zaidi jambo linalomfanya ajivunie filamu hiyo kwani amefanya
kazi kubwa kuanzia uandishi wa muswada wake, huku pia akiwasifia
waigizaji wake kuigiza katika kiwango cha juu, wasanii
walioshiriki katika filamu hiyo ni Rose Ndauka, Salum Haji aka Mboto
mchekeshaji anayefanya vizuri katika filamu hasa sehemu za kuchekesha.
No comments:
Post a Comment