Wednesday, July 24, 2013
FATUMA WA SEGERE AZIKWA LEO BAGAMOYO
Akizungumza na mtandao huu Meneja wa bendi ya Segere bwana Masharubu alisema marehemu alifariki jana katika hospitali ya Muhimbili na alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kifua kwa muda yaliyopsababisha hadi jana kifukia umauti wake.
KELLY ROWLAND ANUSURIKA KUFA MAJI
Mwanamuziki wa miondoko ya R&B, Kelly Rowland ameokolewa kwenye bahari mara baada ya kukwama baharini kwa masaa 12.
Rowland akiwa na watu wengine kadhaa walikutwa na kisanga hicho wakati wanashuhudia maonyesho yaliyofanyika ndani ya boti moja mnamo siku ya Ijumaa asubuhi (July 19th) na gafla hali ya hewa ikabadilika na kusababisha mawimbi makali.
Kepteni wa boti hiyo alipatwa na wasi kutokana na hali ilivyobadilika, ila kepteni wa wa boti ya TowBoat U.S. aitwaye Noah Santos alifanikiwa kumuokoa kila mmoja aliyekuwa kwenye boti hiyo akiwemo mwanamuziki huyo wa ngoma ya “Sail On”.
Santos alisema “kila mmoja alikuwa anatetemeka.” Na baada alipokea asante ya moja kwa moja toka kwa Kelly Rowland:
“Tulitoka naye siku inayofuata nikiwa na mke wangu kisha akatununulia chakula cha usiku. Aliniambia kwamba mimi ni shujaa wake.”
Mpaka sasa aakuna kauli yoyote toka kwa Kelly Rowland au timu yake kutokana na tukio hilo.
Hebu cheki picha ya Kelly akiwa na muokozi wake, Noah Santos..

Posted by
Dan Chibo
Thursday, July 18, 2013
RAY C AWA KIBONGE
Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake.
Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka.
UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga.
Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.
Ray C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza zenyewe.
HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.
Kwa mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia kimatibabu.
Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa , alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu
RAYUU:SIKO TAYARI KUFANYA DHAMBI KWENYE MWEZI MTUKUFU.
Muigizaji wa filamu Rayuu amesema kuwa katika mwezi huu
mtukufu wa Ramadhani anapenda kumcha mungu na hapendi kufanya dhambi
kabisa licha ya watu wachache kutaka aonekane mbaya mbele ya jamii.
Akichonga na Swahiliworldplanet alisema "Mh... Cpendi kufanya dhambi kabisaaa ndo maana mwezi wote najitahidi kuwa msafi na kumcha mungu. Msafi kimatendo ingawa siku zote matendo yangu ni masafi bali tuh wachache ndo hunifanya nionekana mbaya"

LULU AKABIDHIWA RASMI TUZO YAKE YA MUIGIZAJI BORA WA KIKE 2012-2013 KUTOKA ZIFF(PHOTOS)
Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni actress maarufu Swahiliwood
amekabidhiwa rasmi tuzo yake ya best actress in Swahili movies kutoka
Zanzibar international film festival ambayo alishinda hivi karibuni.
Ukiachilia tuzo hiyo Lulu pia alipewa kiasi cha pesa ingawa hatukuweza
kujua ni kiasi gani ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa washindi wa tuzo hizo
kama anavyoonekana pichani hapo chini.
Hongera Lulu na kwa washindi wote wa ZIFF. angalia picha.........................
Wednesday, July 10, 2013
AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA S.AFRIKA
HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wetu jana,
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,
Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
hizo zilionyesha kuwa
wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita
wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa
wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo
yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia
zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi
milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Baada ya kukamatwa na dawa hizo
wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki
moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza
kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.
Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la
Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani
na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia alisema katika kipindi hicho,
Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika
Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania
wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri
kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda alisema mwaka huu pekee
kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa
la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.
Alisema vitendo hivyo vinafanya
vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za
ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu
wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani
RECHO:SIJIPUNGUZI ILI NIOLEWE
MSANII anaye fanya tasnia ya filamu
nchini Recho Haule amefunguka kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa sasa ili kuimarisha mwili na si kwamba anapunguza uzito ili aolewe kama baadhi ya watu wanavyodai.
Nyota huyo mefunguka hivyo baada ya kuibuka tetesi zilizotufikia katika blog hii kutoka kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo ya filamu.
"Kwa sasa nafanya mazoezi kwaajili
ya kutunza hali ya afya yangu,nimekuwa
nikifanya mazoezi ilikuutunza
mwili wangu uwe katika hali ya afya
njema,"alisema Recho .

Subscribe to:
Posts (Atom)