Saturday, April 20, 2013

KAJALA AKIRI KUMKOSEA MAMA YAKE.


Kajala ametoka kukumbana na kashikashi katika maisha yake hivi karibuni, baada ya kusota jela takriban mwaka mmoja kutokana na kesi ya kutakatisha fedha iliyomwandama yeye na mumewe ambaye yuko jela.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Take One’ kinachorushwa kila Jumanne na Clouds Tv, Kajala alisema alipokuwa jela alimkumbuka mama yake kwa mambo aliyokuwa akimwambia na kuanza kujuta kutokana na mateso aliyokutana nayo huko.
 
           “Mimi nilianza kumkumbuka sana mama yangu alivyokuwa akiniusia kutulia, ila mimi natoroka nyumbani nakwenda ninakotaka na kumuacha katika huzuni, ila nilipokaa jela niliona nini umuhimu wa mama, namuomba anisamehe sikujua nilitendalo,” alisema Kajala
 
Aidha, Kajala alisema katika familia yao, mama yake alikuwa ni mkali kuzidi baba yake, ambaye kila kitu walichotaka kufanya aliwaruhusu, ikiwa ni pamoja na kwenda katika majumba ya muziki, lakini mama yao alikataa na kudai sasa anatambua umuhimu wake.

           Aliwashukuru wote ambao walikuwa naye bega kwa bega hadi kufanikisha kutoka jela, huku shukrani za pekee akizimwaga kwa msanii mwenzake Wema Sepetu ambaye alimnusuru kufungwa jela miaka saba kwa kumlipia faini ya sh milioni 13.

Thursday, April 18, 2013

DAVINA APATA MTOTO WA KIUME



 
Msanii wa filamu nchini Halima Yahya 'Davina' amejifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
 Davina amejifungua jumapili katika hospitali ya Agha Khan na anamshukuru mungu amejifungua salama na amerudi nyumban kwa mumewe anayeishi naye sasa Tabata.
“Namshukuru sana Mungu nimejifungua salama, nilimwomba iwe hivyo. Kwa sasa namwomba Mola amjalie afya njema na maisha marefu mwanangu" Alisema.


 

LULU ATIMIZA MIAKA '18'



Lulu akimlisha keki mdogo wake

Akipakua chakula kwenye sherehe yake.
 

Tuesday, April 2, 2013

SUMATRA YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA NAULI


      Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imetangaza viwango vipya vya nauli za mabasi ya masafa marefu, daladala katika jiji la Dar es Salaam, nauli za usafiri wa reli ya kati na bandari.
      Viwango hivyo vimetolewa kutokana na SUMATRA kufuatia maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na makampuni binafsi nchini kutokana ongezeko la gharama za uendeshaji.
       Ahmad Kilima ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa SUMATRA amesema viwango vipya vimetolewa baada ya kufuata taratibu za kisheria na utendaji kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu ongezeko la nauli.
      Amesema SUMATRA imeongeza viwango vya juu vya nauli ya daladala kwa wastani wa asilimia 24.46 na mabasi ya masafa marefu viwango vimeongezwa kwa asilimia 20.3
Pia amesema ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, mamlaka imewataka wamiliki wa mabasi kutotumia wapiga debe katika kuuza tiketi za usafiri na kwamba watakaokaidi hatua za kisheria zitachukuliwa.
       Bwana Kilima amesema katika kufanya mapitio ya gharama mbalimbali za bandari na bahari kuu mamlaka imeridhia ongezeko la gharama kwa wastani wa asilimia 34.3 hivyo TPA wametakiwa kuboresha huduma kwa wateja kwa kuanzisha kitengo cha huduma kwa wateja .
        Hata hivyo ongezeko hilo la nauli limeenda sanjari na viwango vya nauli kwa usafiri wa abiria wa reli ya kati ambapo mamlaka imewataka abiria kukata tiketi na kupanda treni wakionyesha vitambulisho…
     Viwango vipya vya nauli vinatarajia kuanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili 2013 ambapo nauli ya mwanafunzi itakuwa shilingi 200 na mtu mzima atalipa shilingi 400 kwa safari za mijini.

Friday, March 29, 2013

GHOROFA LAUA NA KUJERUHI BAADA YA KUPOROMOKA


Kwa maelezo ya shuhuda, inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.

Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti nne.

Sehemu ya chini zinaonekana bado nzima hazijadondoka ila kifusi cha kutoka juu ndio kimefunika lakini kuna watu ndani yake wako hai na inaripotiwa wanapata hewa vizuri na wamekua wakiwapigia ndugu zao na kuwaita waje kwenye eneo la tukio.

Endelea kuwa karibu nasi kwa habari zaidi.Picha kwa hisani ya Millard Ayo.com

Saturday, March 23, 2013

MICHAEL JORDAN ADAIWA KUKWEPA MAJUKUMU

 



Sakata la Michael Jordan la kudaiwa kukwepa kubeba majukumu
ya kumlea mtoto wake limechukua sura mpya baada ya mama
 wa mtoto huyu, Pamela Smith kupeleka maombi maalum kwa Jaji
 wa kesi hii kumtaka atoe amri ya kufanya vipimo vya DNA kati
 ya Jordan na mtoto wake.
Hatua hii imekuja baada ya Jordan kukataa kuwahi kumlea
 mtoto huyu ambaye anatambulika kwa jina Grant Taj Reynolds
aliyezaliwa mwaka 1996
.
Katika nyaraka mpya ambazo Pamela Smith ameziwasilisha,
mwanamama huyu ameandika kuwa ana uhakika kuwa
Michael Jordan ndiye baba halisi wa mtoto wake kwa sababu
 hesabu zake zinaonyesha kuwa miezi 9 kamili kabla ya kujifungua
 mtoto wake alilala na nyota huyu wa zamani wa mpira
wa kikapu.
Bado Jaji ajatoa maamuzi mpaka sasa kuhusiana na hatua
 ambayo itaamua hatma ya nyota huyu na familia mpya ambayo
inawezekana kuwa ni ya kwake.


Thursday, March 21, 2013

FILAMU YA MWISHO YA KANUMBA YAZINDULIWA SIKU YA KUMBUKUMBU YAKE YA MWAKA1

 
Kanumba-Movie-ya-mwisho-kabla-ya-kufariki
     Tarehe 7/4/2012 ndiyo siku ambayo marehemu Steven Kanumba alifariki dunia, kwenye kumbukumbu yake mwaka huu kutakuwa na uzinduzi wa filamu ya mpya ya Kanumba titled “Love and Power”.
      Hii ndiyo movie ya mwisho Kabisa ya Kanumba ambayo siku hiyo kutakuwa na misa ya kumuombea kwenye kanisa la Kimara na baada ya hapo mambo yatahamia Leader’s Club. Hapo leaders kutakuwa na uzinduzi wa movie hiyo kwa watu wote ambapo hakutakuwa na kiingilio.

       Seth Bosco ambaye ni mdogo wake Steven Kanumba ameelezea siku hiyo kama ifuatavyo,”Itakuwa ni siku ambayo tutatimiza mwaka mmoja baada ya mpendwa wetu Kanumba kufariki dunia, kumbukumbu yake itaenda pamoja na misa ya kuombea na baadaye uzinduzi wa filamu yake moya inaitwa Power and Love. Watu wote mnakaribishwa kwasababu hakutakuwa na kiingilio chochote siku hiyo”