ISHU YA PICHA ZA JACK WA CHUZI LACHUKUA SURA MPYA
BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack
Chuz’ kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo
hiyo ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon
Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya shirikisho hilo kilitonya kuwa, Mhe. Makalla alimvaa Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii
uliofanyika ndani ya Hoteli ya Kibadamu, Ubungo jijini Dar.
“Mhe.
Makalla ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba
kuhusu hatua walizochukua kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa
alinaswa akienda kuuzwa.
“Mwakifwamba alijitetea kuwa, wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama
cha Waigizaji Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako
katika mchakato wa kulitolea uamuzi tukio hilo lililofanywa na Jack ,”
kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi Mwandishi wetu
alimtafuta Mwakifwamba lakini hakuweza kupatikana mara moja ila Mike
alipoulizwa juu taarifa za Mhe. Makalla kucharukia ishu ya Jack alisema:
“Ni kweli waziri aliuliza kuhusu hatua tulizozichukua kuhusu suala la
Jack kujiuza ambapo nilimjibu kuwa tuko kwenye mchakato wa kulitolea
uamuzi na kwa sasa tumeunda kamati maalum, ikimaliza uchunguzi wake
ndiyo tutatoa jibu kuwa tumemchukulia hatua gani.”
No comments:
Post a Comment