Wednesday, October 9, 2013

KARAN JOHAR: HAKUNA KAMA KUCH KUCH HOTA HAI

MWIGIZAJI kutoka Bollywood India Karan Johar amekiri kuikubali sana filamu ya Kuch Kuch Hota Hai, kwa kusema ni filamu ya karne.

Akizungumza na mtandao wa India Express Johar alisema amewahi kutunga na kucheza filamu nyingi lakini hakuna ambayo inapita filamu hiyo kati ya zoote.


Johar alisema amewahi  kucheza na kuandaa ila filamu ya Kuch Kuch Hota Hai ndio filamu yake bora katika soko la filamu la Bollywood.

"kwangu Kuch Kuch Hota Hai ni filamu ya karne ni ya muda mrefu ila bado ndio filamu yangu bora katika soko la filamu la India mpaka leo"Alisema Johar
 

No comments:

Post a Comment