Tuesday, January 22, 2013

SHILOLE NA STYLE MPYA YA NYWELE

     Bongomovie na msanii wa bongofleva Zuwena au Shilole au 'Mtoto mzuri amebadili mtindo wa nywele kwa kukata nywele na kuweka blich sehem ya kati(kiduku).Shilole alisema kuwa alikata kuwa alikata nywele siku ya jumapili ikiwa ni muonekano wake mpya kwa mwaka huu 2013.

MSONGO YAPATA MWANAMUZIK MPYA

Waimbaji wa bendi ya Msondo Ngoma wakiwajibika katika onyesholake maalum la kumtambulisha mwimbaji wao mpya Othumani Kambi(wa pili kulia)wengine ni Hassan Tx Moshi(wa kwanza kushoto)akifuatiwa na Eddy sana na Juma Katundu.Onesho hilo lilifanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni.


Mashabiki wa Bend ya msondo wakicheza kwa furaha wakati wa onesho hilo

Monday, January 21, 2013

MAZUNGUMZO UWANJA WA NDEGE

    Mama Salma Kikwete(wa kwanza kulia) akibadilishana mawazo na Mke wa Rais wa Mali,Mama Toure Lobbo Traore aliyekutana naye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris Ufarasa baada ya kuwasili kwa ziara za Kiserikali ya siku tatu (picha na Ikulu)

KUKANYAGA BUSTANI IKULU

      Askari Polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi wakazi wa Dar es salaam wenye asili ya China,baada ya kuwakamata kwa kosa la kukanyaga bustani inayozunguka eneo la Ikulu kwa gari lao, jijini Dar es salaam juzi(picha na Yusufu Badi).

UKUTA WA UBUNGO WAANGUKA NA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA

    Leo alfajiri ukuta wa Stand ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo jijini Dar es salaam umeanguka nakuzusha hofu kubwa kwa wasafiri.
    Inadaiwa kuwa watu wanne wamejeruhiwanhuku magari 24 yaliyokuwa yameegeshwa mahali hapo yakiharibiwa vibaya na ukuta huo.
    Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alipokuja eneo la tukio alisema chanzo cha ajalini mkandarasi aliyekuwa akibomoa ukuta bila tahadhari.
     Hizi ni baadh ya picha za tukio hilo kwa hisani ya mtandao wa global.




JUISI YA EMBE NA PASSION

  Juisi ya embe na passion ni juisi rahisi kuandaa na pia ni juisi zuri kiafya.Unaweza kutengeneza kwaajil ya nyumbani au unaweza kubeba kwaajil ya kazini kuliko kununua juisi ambazo zina kemikali ambazo sio nzuri kwa afya.
      Mahitaji
Passion fruit                                                            8

Embe                                                           6 za kiasi

Maji                                                                       kiasi

Sukari                                                                   kidogo

       Namna Yakuandaa.
1.   Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji   kiasi kisha saga na uchuje .

2.   Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion.

3.   Tia sukari kidogo  ikiwa tayari kwa kunywewa.

      Lakini unaweza kutumia mchanganyiko  wa maembe na ma'passion kula bila kusaga mana vinakazi moja katika mwili wako.
      Unapata vitamini na inakukusaidia kupata choo vizur na faida nyinginezo.
 

Sunday, January 20, 2013

FASHION YA VIATU KWA WANAWAKE

     Katika vitu ambavyo wanawake au wasichana wapenda mitindo wanaziangatia ni pamoja na viatu hasa vilivopo kwenye vinavyoenda na wakati.
     Kuna viatu kwaajili ya harusi,kazi,mitoko ya jion.na sehem nyenginezo.Vipo virefu na flat.
          Vifuaatavyo ni baadhi ya viatu vyakisasa kwa wasichana