Wednesday, May 1, 2013

NSHOMA WA BSS AELEZA SABABU ZA UKIMYA WAKE

MSANII aliyeshiriki mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji bongo star search(BSS)  mwaka jana Nshoma Ng'hangasamala Nkwabi aeleza sababu za ukimya wake baada ya mashindano hayo.Nshoma ni mmoja wa walioingia katika tano bora wakati wa kinyang'anyiro,na kuwa kivutio kwa kuimba nyimbo mbalimbali za asili ya kiafrika,

Akizungumza na Keshe hivi karibuni Nshoma alisema ameamua kuwa kimya ili aweze kutunga nyimbo zitakazoweza kuendana soko na kuweza kudumu kwa muda mrefu."Haraka haraka naamini haina baraka hivyo nimeamua kutulia ili niweze kutoa nyimbo zuri zitakazoweza kudumu kwenye soko kwa muda mrefu na ziwe bora kama nyimbo za Mariam Makabe ambaye nakubali mno kazi zake"Alisema.

Nshoma alisema kwa sasa anafanya kazi zaidi ya uimbaji na unenguaji kwenye bendi yake mwenyewe na atakua anauza albamu zake kwenye  shoo atakazokua anafanya akiwa na  bendi hiyo."Nataka niuze mwenyewe kazi zangu na nitakuwa naziuza kwenye shoo nitakazokua nafanya na bendi yangu,hivyo mashabiki wanahudhuria ndio watakaokuwa wananunua albamu zangu" alisema.
Pia Nshoma alieleza mafanikio mengine aliyoyapata baada ya shindano ikiwa ni pamoja na mkataba wa kila mwaka kufundisha kucheza na kupiga ngoma katika shule ya Music shule iliyopo Ujerumani, shavu la kutunga nyimbo kuhusu katiba mpya na wanawake, mkataba wa kufundisha warembo wanaowania taji la mrembo wa Bagamoyo na kuunda kundi la muziki pamoja na ndugu zake linaloitwa 3sisters.
Nshoma alisema kazi nyingi anazifanya pamoja na familia yake ambapo wanashirikiana katika uimbaji pia yupo dada yao ambae ni mshauri mkubwa mshauri wake mkubwa na baba yake ndiye msimamizi wa kazi zake zote.

Nshoma ni msanii kutoka bagamoyo akiwa anaimba nyimbo za asilia na anayetokea katika familia ya vipaji ikiwa baba yake ni mwalimu wa chuo cha sanaa bagamoyo,mama yake ni mpiga kinanda na yeye pamoja na ndugu zake wakiwa ni wasanii.

 

Tuesday, April 30, 2013

BABA CHRIS BROWN AVUTIWA NA HUYU KUWA MKWE NA SI RIHANNA

 

Gazeti la New York Daily News limefanya Exclusive interview na baba mzazi wa mwimbaji staa Chris Brown na kutoa maoni yake kuhusu mahusiano ya kimapenzi ya mwanae na Rihanna RiRi.

Clinton Brown amesema “sioni maisha marefu kwa Chris Brown kuwa na Rihanna, sijawahi kupendezwa na kurudiana kwao, unajua ni lazima kwenye uhusiano wa kimapenzi uwe na mtu sahihi ambae ni hitaji la kweli na linaloweza kuwa lako kwenye maisha, lakini sio kama hivi”

Clinton amesema hapendi kutumia mifano lakini anadhani watu wameona mahusiano ya mastaa kama Whitney Houston, Michael Jackson, Amy Winehouse na wengine”

Kuhusu mrembo ambae angependa kuona anaolewa na mwanae, Clinton amemtaja Jordin Sparks kwa kusema “nimempenda Jordin, ni msichana mdogo lakini mwenye upeo mkubwa… ana akili na heshima

HAMMER Q AMSHUSHIA MKEWE KIPIGO KISA HASSAN TX MOSH

 Hammer Q akiwa na Mkewe siku ya harusi yao.
 
zifuatazo ni baadh ya picha za Salha akiwa na majeraha

Msanii wa Taarabu wa kundi la Five Star na kundi la Off Side Trick amempiga mke wake wa ndoa kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Salha mke wa Hammer Q ambaye pia ni msanii anayeunda kundi la Dar es Salaam Modern Taarabu alisema mumewe alianza kumpiga walipokuwa katika show ya kundi la Five Star iliyokua inafanyika Dar Live Mbagala jijini Dar es salaam.


Akizungumza na Clouds Fm kwa njia ya simu alisema amelazwa katika hospital baada ya kupigwa alisema walipokuwa Dar Live Salha alionana na Hassan Tx Mosh akamtambulisha kwa mumewe ambaye ndipo Hammer alipoanza kumpiga kwa kusema kwanini ametambulishwa.

"mimi sikuona tatizo kumtambulisha lakin baada ya hapo alitaka tuondoke tulipofika nyumbani kipo alipoanza kunipiga sana amenichana sana mgongoni,mikononi,usoni na hapa nimeshonwa nyuzi nyingi"

Baadh ya mashuhuda ikiwepo mwenye nyumba wao alisema walimsihi sana aache kumpiga mkewe lakini alisema yule ni mkewe na alilipa pesa hivyo hataki mtu aiingilie.

"watu walimsihi sana asinipige lakin alikataa alinipiga mpaka na jiko la uso na ameniharibia sana vitu vyang ndani kwang yani sijui kama ntaweza kurudiana tena mana si mara ya kwanza"

Lakini alipotafutwa Hammer Q alisema ilikua ni hasira na walikua wamelewa hivyo ni pombe tu.

Kesi imeshafika polisi na wazazi wa Salha wanafuatilia na Hammer Q hajulikani alipo mpk sasa.

Uongozi wa Blog hii unalaan vikali vitendo kama hivi mana ni unyanyasaji wakijinsia.

Endelea kufuatilia Blog hii kuweza kujua kitakachoendelea

Monday, April 29, 2013

TUNDAMAN ATOA YAMOYONI KUHUSU STYLE YAKE MPYA YA NYWELE



Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye pia ni mshiriki wa kundi la Tip Top Connection Tundaman ameamua kuongea ya moyoni baada ya baadhi ya mashabiki wake kuponda staili yake mpya ya nywele kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza na gazeti hili Tundaman alitoa sababu zakuweka staili hiyo ya nywele ambapo alieleza kuwa mcheza sinema maarufu anayemuhusudu aitwaye Tom Po ndiye anaweka staili hiyo ya nywele siku zote.

Tundaman alisema amekua na muonekano wa kawaida kwa muda mrefu hivyo ameamua kuwa na mpya na hiyo ndiyo sababu iliyochangia yeye kuweka stail hiyo ya Tom Po .



"Nimekua na staili moja ya nywele siku nying hizo nimependa niwe na muonekano mpya  sababu nampenda sana Top Paul na mara nyingi naangalia filamu anazocheza na kwakua siwezi kuigiza kama yeye ndio maana nikaamua kuweka staili hii ili kuonyesha mapenzi yangu kwake"Alisema.

Aliongeza kuwa" Hata Lil Wayne alipoamua kuchora tatoo mwili mzima baadh ya mashabiki walimsema vibaya lakini sasahivi wamezoea na maisha yanaendelea hivyo kwang pia watazoea"

Hata hivyo alisema kuwa tayari ameshaitambulisha nyimbo yake ya 'wanaona haya' aliyoshirikiana na Chege na video wanaenda kuifanya katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
 

Saturday, April 20, 2013

KAJALA AKIRI KUMKOSEA MAMA YAKE.


Kajala ametoka kukumbana na kashikashi katika maisha yake hivi karibuni, baada ya kusota jela takriban mwaka mmoja kutokana na kesi ya kutakatisha fedha iliyomwandama yeye na mumewe ambaye yuko jela.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Take One’ kinachorushwa kila Jumanne na Clouds Tv, Kajala alisema alipokuwa jela alimkumbuka mama yake kwa mambo aliyokuwa akimwambia na kuanza kujuta kutokana na mateso aliyokutana nayo huko.
 
           “Mimi nilianza kumkumbuka sana mama yangu alivyokuwa akiniusia kutulia, ila mimi natoroka nyumbani nakwenda ninakotaka na kumuacha katika huzuni, ila nilipokaa jela niliona nini umuhimu wa mama, namuomba anisamehe sikujua nilitendalo,” alisema Kajala
 
Aidha, Kajala alisema katika familia yao, mama yake alikuwa ni mkali kuzidi baba yake, ambaye kila kitu walichotaka kufanya aliwaruhusu, ikiwa ni pamoja na kwenda katika majumba ya muziki, lakini mama yao alikataa na kudai sasa anatambua umuhimu wake.

           Aliwashukuru wote ambao walikuwa naye bega kwa bega hadi kufanikisha kutoka jela, huku shukrani za pekee akizimwaga kwa msanii mwenzake Wema Sepetu ambaye alimnusuru kufungwa jela miaka saba kwa kumlipia faini ya sh milioni 13.

Thursday, April 18, 2013

DAVINA APATA MTOTO WA KIUME



 
Msanii wa filamu nchini Halima Yahya 'Davina' amejifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
 Davina amejifungua jumapili katika hospitali ya Agha Khan na anamshukuru mungu amejifungua salama na amerudi nyumban kwa mumewe anayeishi naye sasa Tabata.
“Namshukuru sana Mungu nimejifungua salama, nilimwomba iwe hivyo. Kwa sasa namwomba Mola amjalie afya njema na maisha marefu mwanangu" Alisema.


 

LULU ATIMIZA MIAKA '18'



Lulu akimlisha keki mdogo wake

Akipakua chakula kwenye sherehe yake.