Wednesday, May 1, 2013

NSHOMA WA BSS AELEZA SABABU ZA UKIMYA WAKE

MSANII aliyeshiriki mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji bongo star search(BSS)  mwaka jana Nshoma Ng'hangasamala Nkwabi aeleza sababu za ukimya wake baada ya mashindano hayo.Nshoma ni mmoja wa walioingia katika tano bora wakati wa kinyang'anyiro,na kuwa kivutio kwa kuimba nyimbo mbalimbali za asili ya kiafrika,

Akizungumza na Keshe hivi karibuni Nshoma alisema ameamua kuwa kimya ili aweze kutunga nyimbo zitakazoweza kuendana soko na kuweza kudumu kwa muda mrefu."Haraka haraka naamini haina baraka hivyo nimeamua kutulia ili niweze kutoa nyimbo zuri zitakazoweza kudumu kwenye soko kwa muda mrefu na ziwe bora kama nyimbo za Mariam Makabe ambaye nakubali mno kazi zake"Alisema.

Nshoma alisema kwa sasa anafanya kazi zaidi ya uimbaji na unenguaji kwenye bendi yake mwenyewe na atakua anauza albamu zake kwenye  shoo atakazokua anafanya akiwa na  bendi hiyo."Nataka niuze mwenyewe kazi zangu na nitakuwa naziuza kwenye shoo nitakazokua nafanya na bendi yangu,hivyo mashabiki wanahudhuria ndio watakaokuwa wananunua albamu zangu" alisema.
Pia Nshoma alieleza mafanikio mengine aliyoyapata baada ya shindano ikiwa ni pamoja na mkataba wa kila mwaka kufundisha kucheza na kupiga ngoma katika shule ya Music shule iliyopo Ujerumani, shavu la kutunga nyimbo kuhusu katiba mpya na wanawake, mkataba wa kufundisha warembo wanaowania taji la mrembo wa Bagamoyo na kuunda kundi la muziki pamoja na ndugu zake linaloitwa 3sisters.
Nshoma alisema kazi nyingi anazifanya pamoja na familia yake ambapo wanashirikiana katika uimbaji pia yupo dada yao ambae ni mshauri mkubwa mshauri wake mkubwa na baba yake ndiye msimamizi wa kazi zake zote.

Nshoma ni msanii kutoka bagamoyo akiwa anaimba nyimbo za asilia na anayetokea katika familia ya vipaji ikiwa baba yake ni mwalimu wa chuo cha sanaa bagamoyo,mama yake ni mpiga kinanda na yeye pamoja na ndugu zake wakiwa ni wasanii.

 

No comments:

Post a Comment