Saturday, May 4, 2013

JACKLINE WOLPER AELEZEA SABABU ZAKUITWA WOLPER GAMBE STYLE


Msanii maarufu wa filamu nchini, Jackline Wolper 'amber Rose wa bongo'aelezea jinsi alivyoitwa Wolper Gambe badala ya jila alilopewa awali la Wolper Gangnam.
 
Akizungumza na Kesheridhiwani BlogSpot alisema jina la Wolper Gangnam lilikuja kutokana na mistari iliyopo kwenye nyimbo ya gangnam style inayosema Opa gangnam sytle.
 
”Mwanzo watu walibadirisha wimbo wa yule mkorea PSY..ukimsikiliza anavyoimba inasikika Opa gangnam style, ikabadilishwa na kuwa Wolper gangnam style kwasababu ina sound sawasawa. Lakini baadae wakabadilisha zaidi na kuimba Wolper gambe style unajua jinsi neno gambe lilivyo maarufu na raisi kulitumia hapo lina sound poa. Sasa wimbo ulivyoanza ku-kick zaidi ndiyo na jina likawa kubwa zaidi,”
 
Wolper alisema wapo baadhi ya watu ambao walidhani yeye alitumia jina la Jackline Gambe kwa sababu ya ulevi lakini amesisitiza sio kweli na ni watu tu walioamua kubadilisha katika utamkaji wake.

No comments:

Post a Comment