Thursday, October 10, 2013

ROSE NDAUKA AKANA KUWA NA UJAUZITO WA MTARAJIWA WAKE.

Mwigizaji wa filamu Bongo Rose Ndauka akana kuwa na ujauzito huku Mtarajiwa wake Malick Bandawe akiwa akidai anafanya kila awezalo ili Rose aenjoy katika kipindi hiki cha ujauzito.

Na Mtarajiwa wake huyo ambaye naye pia ni Msanii wa Bongo fleva alipoulizwa kuhusu Ndoa alisema anasuburia  mpaka atakapojifungua mana kwa imani ya dini yake haruhusiwi kuoa mke ambaye ni mjamzito.

Zifuatazo ni baadhi ya picha wakiwa katika Hotel yenye hadhi ya Nyota tano.
 
 

MTOTO WA STELLA DAMASUS AKINGIA KWENYE UIGIZAJI.

Stella Damasus.
Binti wa mwigizaji maarufu wa Nigeria Stella Damasus ameingia kwenye fani ya mama yake.

Stella bila kutaja jina aliandika katika ukurasa wake wa Twitter
kuwa binti yake huyo atakuwa akionekana pia katika mtandao wa MixMatch, utakaokuwa ukirusha matukio ya kifamilia yatakayoandaliwa kama filamu kutoka New York marekani.

Stella Damasus ambaye pia ni muimbaji hajawahi kuzungumzia chochote kuhusu kuhusu ama kutokuwa tayari mtoto wake huyo kuingia katika fani yake ya uigizaji.

CHEZEEEAAA MADAM WEMA!!!

Hii imekuja baada ya Diamond ku-post katika account yake ya Instagram kua wako katika Zoezi la kushoot movie mpya iitwayo TEMPTATIONS yeye na Wema  huko China. Haya tusubiri tuone mana hata Penny tuliambiwa wanashut muvi mpyaaaaaaaaaa ikwa muviiiiiiii!!!!
Wema akiwa na Diamond katika moja ya mitaa huko Hong Kong China.
 

Wednesday, October 9, 2013

CHRISTINA MILIAN ASEMA PENZI LAKE KWA JAS PRICE NI LA MILELE

 

Mwanamuziki na mwigizaji Christina Milian amefunguka kuhusu penzi lake kwa Jas Price akiweka wazi kwamba ni la milele na hakuna wa kulivuruga.

Milian alisema mtu yeyote hawezi kuvuruga penzi lao kwa namna yeyote ile kwani ni uhusiano wa muda mrefu ambao wameweza kudumu kwa muda wa miaka mitatu.

"Jas ajanivisha pete lisha ya kuwa kwenye uhusiano naye kwa muda wa miaka mitatu, lakini naamini hiyo siyo ishara ya kunichoka na kuvunja uhusiano wetu"Alisema Milian.

KARAN JOHAR: HAKUNA KAMA KUCH KUCH HOTA HAI

MWIGIZAJI kutoka Bollywood India Karan Johar amekiri kuikubali sana filamu ya Kuch Kuch Hota Hai, kwa kusema ni filamu ya karne.

Akizungumza na mtandao wa India Express Johar alisema amewahi kutunga na kucheza filamu nyingi lakini hakuna ambayo inapita filamu hiyo kati ya zoote.


Johar alisema amewahi  kucheza na kuandaa ila filamu ya Kuch Kuch Hota Hai ndio filamu yake bora katika soko la filamu la Bollywood.

"kwangu Kuch Kuch Hota Hai ni filamu ya karne ni ya muda mrefu ila bado ndio filamu yangu bora katika soko la filamu la India mpaka leo"Alisema Johar
 

Friday, September 27, 2013

PEEPLES...HII NDIO MOVIE AMBAYO WIMBO WA SAIDA KALORI CHAMBUA KAMA KARANGA UMETUMIKA.

Wengi tulioangalia movie hii ya Marekani tumejiuliza wimbo wa Saida Kalori umewafikiaje.Maana ukiangalia movie hii mwanzoni mwanzoni kabisa wimbo chambua kama karanga unasikika na anaonekana mama akiucheza kama sehemu ya mazoezi.
Saida Kalori  hakua akijua chochote kuhusu nyimbo yake kutumika katika movie hiyo.Pia aliyewahi kuwa manager na producer wa Saida hakuwa akijua chochote zaidi ya kupigiwa simu kutoka Marekani na wanawe waliyoiona movie hiyo. 


Zifuatazo ni baadhi ya picha za movie hiyo







Chanzo:Dina marios, blogspot
 

Thursday, September 26, 2013

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUPAKA MAKE'UP

Vipodozi au Makeups ni urembo unaopendwa zaidi na wanawake wengi, dhamira yao ikiwa ni kubadili muonekano wao uliozoeleka ili wapendeze.

Mara nyingi watu wanapopaka makeups tofauti hujitokeza usoni kutokana na kipodozi hicho kufanya kazi ya kung'arisha na kupendezesha uso.

Unapofika wakati wa kupaka makeups,kwanza unapaswa kuchagua ni ipi itakufaa na kukupendeza. swali la kam kipi kitafaa zaidi kati ya poda au cream,hilo linabaki kwa mhusika kwa kuwa kila mmoja anapendekezo lake,kutokana namna anavyopata matokeo mazuri.


MAMBO YAKUZINGATIA KABLA YA KUPAKA MAKEUPS.

Kwanza jaribu kutafuta make ups inayoendana na ngozi yako na rangi ya mwili wako.

Watu wenye ngozi za mafuta wanashauriwa  kupaka makeup ya poda au unga unga kwani ya cream inaweza kuziba vitundu vya hewa katika ngozi ya uso.

Kwa walio na ngozi kavu wafahamu kuwa, make up ya cream haina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu katika ngozi hivyo kama unahitaji kuwa nayo kwa muda unaozidi masaa nane unapaswa kupaka makeup ya poda iliyozoeleka na wengi.

Hakikisha unapaka makeup kwa kutumia brash zake maalum na si kitambaa au mikono.