Friday, February 8, 2013

WEMA SEPETU AVAMIA PENZI LA MISS TANZANIA.


BAADA ya Msanii  wa Filamu nchini Tanzania Wema Sepetu kukaa kimya muda mrefu bila kuwa na mikiki ya wanaume, mwana dada huyo mwenye mvuto wa mapenzi kwa wanaume ameibuka tena katika dimbwi la mahusiano mapya na Serengeti boy ili kulipiza kisasi kwa X wake wa zamani,  Abdul Nasibu Juma (Diamond Platinum).....

Pamoja na hisia za mapenzi za mwanadada kuyo kusumbua wanaume wengi lakini amekosa bahati ya kutimiza ndoto zake za kutulia kimapenzi na mpenzi mmoja kama walivyo baadhi ya wanawake wenzake.

Taarifa zilizonaswa  zinadai kwamba hivi sasa Wema anadaiwa kuzama kwenye mahaba na Haidary Cavilla ambaye ni mchumba wa miss Tanzania namba 2 ,mwaka 2000, Mercy Galabawa, hata hivyo inadiwa kuwa kidume hicho aliyefanikiwa kumchanganya msanii huyo kwa mkwanja mrefu ni mdogo kiumri zaidi ya Wema.

Hata hivyo chanzo cheti cha habari kimezidi kudokeza kwamba bwana mdogo huyo amemchanganya Wema baada ya kununuliwa gari aina ya Audi Q7.....wadau wa karibu wa Wema pia wanadai kwamba Wema ameamua ku-break picha walizopiga na mpenzi wake huyo mpya nyumbani kwa Wema kwenye mitandao ya kijamii akiwa na lengo la kulipiza kisasi wa  Diamond Platinum. 

Wema Sepetu ni kati ya warembo wachache nchini wanaokabiliwa na visa vya kubadili wanaume kama nguo kwani mpa hivi sasa amekuwa na idadi ya wanaume wanane waliojulikana hadharani  1. MR BLUE 2.TID 3. Marehemu STEVEN KANUMBA 4.JUMBE YUSUPH JUMBE 5.CHAZ BABA 6.DIAMOND PLUTNUM 7. CLEMENT ( Bado wako pamoja) 8. HAIDARY CAVILLA

No comments:

Post a Comment