Wednesday, February 20, 2013

MWANA'FA' KUANZISHA RECORD LABEL


Ni miaka zaidi ya kumi tangu hamis mwinjuma atie maguu kwa mara ya kwanza kwenye game ya muziki wa kizazi kipya na ngoma yake ya ingekua vipi, Mwana FA ame surport wasanii wengi kwa kupiga nao collabo kwenye ngoma zao, lakini this tyme ameenda more miles kwa kuanzisha record label, na tayari ame sign vichwa kadhaa na hivi karibuni label hiyo ime release ngoma ya msanii wake mmoja, mwanadada anaitwa maua, pini linaitwa Crazy feat yeye mwenyewe

"niliona naweza kutoa mkono sasa, nimefanya mziki kwa mda mrefu na siwezi kumsaidia kila mmoja anaefanya mziki, kuna watu wanavipaji vinapotea mtaani huku, na nikaona naweza kufanya kitu, kwahiyo tutakua very selective, maana hatutaki kuwa na watu wengi kwenye lebo tukashindwa kusambaza kazi zao
tutachagua wawili watatu ambao tutaona vipaji vyao vinajitosheleza na kuwasimamia haitatupashida, maua ndio ameanza sema kuna wengine wawili watatu mnawajua ila maua tumeona ndio wakati wake, na muda haujafika wa sisi kuwataja na kuanza nao kazi rasmi hadharani, bado tunafanya kichinichini"

"lebo ina kama mwaka hivi lakini tunaendesha shughuli kichinichini, tunajaribu  ku scout watu, kupanga mambo yetu, kusajili kampuni yaani utaratibu wa nyuma kabla mziki haujaskika na mtu wa kwanza kutoka ni maua kwasababu muda wake umefika na niwakati wa kipaji chake kukipeleka mbele na sio cha kukilazia damu au kulala nacho"amesema  FA baada ya kuulizwa lebo imekuwepo kwa muda gan.

No comments:

Post a Comment