Friday, February 22, 2013

UNAWEZA KUANDAA CHAKULA HIKI KWA AJILI YA MLO WAKO.

Viazi Vya Nazi Kwa Nyama


     
 
Vipimo
Viazi                              1kilo
Nyama                           1/2
Kitunguu                        1
Nyanya                          2
kitunguu saumu            1 kijiko cha chai
Manjano                        ½ kijiko cha chai

Nyanya kopo                  1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga                  kiasi upendavyo
Chumvi                           kiasi
Tui la nazi                      kikombe1 cha chai
Mtindi ukipenda              3 vijiko vya supu
Kotmiri                           kiasi ya kupambia
Nazi ya unga                  4 vijiko vya supu
Mafuta                           2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive.
  2. Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni
  3. Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi
  4. Tia kitunguu saumu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo
  5. Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu.
  6. Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini    visiwe vikavu.
  7. Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.

No comments:

Post a Comment